HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 May 2013

TBF KUINGIA KANDARSI YA MUDA MREFU NA Albert Sokaitis


 

Mkufunzi wa mchezo wa mpira wa kikapu kutoka Marekani  Albert Sokaitis alitarajiwa kuwasili jana usiku jijin Dar es Salaam baada ya kualikwa na Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania .

Katibu mkuu wa msaidizi wa shirikisho hilo  Michael Maluwe amesema mkufunzi huyo atasaini kandarasi yake wiki hii lakini akuweka wazi kuwa itakuwa wa muda gani ,

Maluwe amesema kuwa mkufunzi huyo atakaa kwa muda mrefu zaidi ili kuusaidia mchezo katika mafunzo mbalimbali ya makocha na wachezaji ili aweze kuuinua mchezo huo Nchini  .

Maluwe ameongeza kwa kusema mengi kuhusu kandarasi  na kazi atakazo fanya zitajulikana na  zitawekwa wazi pale atakapo wasili  .


Rais wa TBF  Musa Mziya akupatikana kuzungumzia swala hilo kwani simu yake ilikuwa imezimwa.

 
Maluwe ameaongeza kwa kusema ujio wa mkufunzi huyo utakuwa ni muhimu sana kwa kuukuza mchezo wa mpira wa kikapu  .
Hii ni mara ya kwanza kwa Shirikisho la mpira wa kikapu kuleta mkufunzi wa muda mrefu ili kuleta changamoto za mpira wa kikapu . Maluwe " TBF inatazama zaidi kuundeleza mpira wa kikapu hasa kwa vijana na mashuleni ili kupata vijana zaidi waweze kuucheza mchezo huo .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers