HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

8 June 2013

Tonny Mawejje AIPA SALAMU LIBERIA AACHIA BAKORA KALI YAMSHINDA KIPA WA LIBERIA

 
Uganda Cranes imejiweka katika nafasi nzuri  Leo katika kufuzu kombe la dunia  2014 Baada ya kuikandamiza  Liberia kwa bao moja kwa bila  katika uwanja wa Mandela jijini kampala 
lakini mechi hiyo iliiisha vibaya kwa kwa timu ya  Liberia baada ya wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na nyota wao  Roberts Omega kumzonga mwamuzi wa mchezo  Adam Cordier kutoka  Chad kwa kile walichodai kuchezesha vibaya kiasi cha kuwafanya wa   kushindwa kuvumulia lakini Liberia na  Bench lake la  ufundi la ilibidi wapunguze hasira ili kutuliza vurugu hizo .
Goli la ushindi liliwapa mashabiki wa Uganda Mdadi wa hari ya juu mara baada ya  Tonny Mawejje  kufunga goli katika dakika ya sita tu ya mchezo  baada ya kuidanganya safu ya ulinzi ya  Liberia na kuachia  bakora kali kali huku safu ya ulinzi  ikishindwa cha kufanya .’ Uganda kwa sasa wanalingana alama na Senegal ambao na wao wanacheza na  Angola huko  Luanda katika Kundi  J. Timu zote zina alama Tano. Huku Liberia ikiwa na Alama  Nne wakati  Angola wao wana Alama  Tatu  .Timu inayoongoza kwa kila kundi itafuzu kwa hatua ya pili ya makundi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers