HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

6 July 2014

BRAZIL HAIJAFUNGWA MECHI AROBAINI NA MOJA KWAO JE ,WAJERUMANI WATAWEZA KUVUNJA REKODI HIYO?




Mpambano huu wa Timu mbili zenye uwezo wa hari ya juu unatarajiwa kuwa moja ya mchezo wa Kuvutia ambapo wa Brazil wakiwa katika mpango kushinda Nishani au medali ya Kombe la Dunia wakiwa Nyumbani wakati wajerumani wao wakitaka kushinda Kombe hilo kwa mara ya kwanza Tangu mwaka  1990.
Baraa Limeikuta kambi ya Brazil ambapo mchezaji wao Hodari kiwanjani Neymar ameondolewa kabisa katika mashindano mara Baaada kupata Mkasa wa Kuvunjika Mfupa wa Uti wa Mgongo unao juilkana kama vertebra ambapo aliumia kwenye mchezo wa Robo fainali katika Timu ya  Colombia. Meneja wa Timu ya Brazil Luiz Felipe Scolari anatazamiwa kuja na suluhisho litakalo ziba pengo hilo,Huku mchezaji kutoka   Barcelona akiwa amefanya kazi kubwa akiwa na Barca katika mechi za Msimu huu,na anatazamiwa kutegemea wachezaji kama  Hulk na Mchezaji wa  Chelsea’s Oscar akitazamiwa kuwa katika kiwango chake cha juu. Ili aweze kuingamiza Ngome ya Timu mpinzani  , Nahodha wa timu hiyo  Tsiago Silva  atakuwa nje akiwa anatumikia adhabu ya kadi ya njano aliyopata katika mechi iliyopita.
Wajerumani wanaonekana kuwa wazuri katika kuutawala mpira tena walioneka wazuri dhidi ya Ufaransa Meneja wa Timu Joachim Low alifurahishwa na timu yake mara baada ya kuonyesha uwezo mzuri baada ya kurejea kiwanjani kwa Mats Hummels, ambae alifunga goli la ushindi. Timu inatarajiwa kuwa na namna hii Thomas Muller, Mario Gotze na Mchezaji toka  Arsenal’s Mesut Ozil kuisumbua Safu ya Ulinzi ya Brazil’s
Timu hizi zimekutana mara tatu katika mechi za kirafiki na matokeo yalikuwa hivi
Germany 3 (Schweinsteiger, Gotze, Schurrle) Brazil 2 (Robinho, Neymar), , August 2011
Germany 2 (Podolski, Ballack) Brazil 3 (Leite 2, Ronaldinho), Confederations Cup, June 2005
Germany 1 (Kuranyi) Brazil 1 (Ronaldinho), , September 2004

Tangu ukuta wa Berlin udondoke , Brazil imekutana na Mara tisa ambapo wamewafunga wajerumani mara tano na wakifungwa mara mbili.
Wajerumani wameingia nusu fainali kwa mara ya kumi na tatu  Tangu mwaka 1966. Na wametinga fainali mara sita katika mara zote hizo.
Mshambuliaji wa Lazio  Miroslav Klose anahitaji goli moja tu kuvunja Rekodi  ya kuwa mfungaji bora katika historia ya michuano ya Kombe a dunia. Kama atafunga katika mechi hiyo basi atampita mfungaji Bora wa Brazil Nguli wa Brazil  Ronaldo, ambapo sasa wanafungana kwa magoli  15 .
Brazil hawajafungwa katika mechi zao 41 za nyumabni. Mechi ya mwisho kufungwa ilikuwa Dhidi ya Paraguay mwaka 2002 ,Goli lilofungwa na Tsiago Silva’s Katika Dakika ya Saba Dhidi ya Colombia lilikuwa Goli la mapema zaidi tangu mwaka 2002  Brazil’s ndio ilifunga goli la mwisho la mapema zaidi  .
Meneja wa Brazil  Luiz Felipe Scolari Hajapoteza mechi ya Kombe la dunia akiwa na Brazil;na alikuwa kocha mara mwisho mwaka 2002 pale  Selecao ilipotwa ubingwa mwaka 2002.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers