HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

20 July 2014

STARS ,YASHINDWA KULINDA MAGOLI HAMIS MCHA SUPA SUB DHIDI YA MSUMBIJI YATOKA SARE 2-2

Timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Imelazimshwa sare ya mabao mawili kwa mawili Dhidi ya Msumbiji  katika mchezo wa kuwania kufuzu Mataifa ya Afrika yatakayofanyika Nchini Morocco mwakani .
ilichukua Dakika moja tu tangu kuanza kwa kipindi cha pili kwa msumbiji kuliona Lango Tanzania kwa Mkwaju wa Penati baada Kelvin Yondani Kumfanyia Faulo mshambuliaji wa Msumbiji na mwamuzi kuamuru ipigwe Penati.
Stars walipigana kufa na kupona mpaka pale alipoingia Hamis Mcha katika dakika ya sitini  badala mrisho Ngasa na kusawazisha Goli hilo kwa mkwaju mkali , Voley kutoka upande mashariki wa kiwanja na kumwacha Mlinda mlango wa msumbiji Ricado Campos asijue cha Kufanya .
Dakika tano Baadae Beki wa timu ya Msubiji alimfanyia Faulo Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayechezea klabu ya Tout Puisant Mazembe ya Congo na kumwachia Jukumu kijana wa Kizanzibar Hamis ncha kufunga Bao la Pili .
Stars iliendelea kulisakama lango la msumbiji na alimanusula ipate bao la tatu pale mpira uliopigwa na samata kugonga mlingoti wa Goli lakini Baadae mlinga Mlango wa msumbuji aliudaka na kuanzisha Kaunta Ataki na kuipatia msumbji goli la kusawazisha lilofungwa na  Isaac Calvaho akipokea pasi kutoka kwa  Domingues baada ya Yondani kupigwa kanzu na kuipatia Sare timu yake .
Timu hizo zitarejeana baada ya majuma mawili Huko maputo nchini Msumbiji.
PICHA BIN ZUBERY

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU

MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers