Mabingwa
wa soka Tanzania bara Azam FC wametangaza dhamira yao ya kutaka kumsajili
kiungo wa klabu ya Simba Amri Ramadhan Kiemba ambae kwa sasa bado anasubiri
hatama yake kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo ya Msimbazi kufutia tuhuma za
kucheza chini ya kiwango katika michezo mitano ya kwanza ya ligi kuu.
Mwenyekiti
wa klabu ya Azam FC, Sheikh Said Muhammad Abeid amesema tayari wameshawasilisha
ofay a kutaka kumsajili Kiemba baada ya kocha wao kutoka nchini Cameroon Joseph
Omog kumpendekeza miongoni mwa wachezajia mbao angependa wasajiliwe katika
kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili..
Hata
hivyo mwenyekiti huo wa Azam FC amesema dhumuni lao kwa kiemba ni kumsajili kwa
mkataba wa mkopo akitokea Simba na si kumsajili moja kwa moja kama walivyoanza
kufanya kwa beki kutoka nchini Ivory Coast Serge Wawa akitokea kwa mabingwa wa
soka nchini Sudan El Merekh.
Katika
hatua nyingine mwenyekiti wa klabu ya Azam FC, Sheikh Said Muhammad Abeid
amekiri kusikitishwa na mwenendo mbovu wa klabu ya Mbeya City ambayo kwa msimu
huu ulioshuhudia michezo saba mpaka sasa imeshindwa kufanya makubwa kama
ilivyokua msimu uliopita ambapo walicheza ligi kwa mara yao ya kwanza.