Abiria 45 waliokuwa wakisafiri katika basi la Abiria kati ya SONGEA na MCHOMORO wilayani NAMTUMBO katika Mkoa wa RUVUMA wamenusurika kufa baada ya basi hilo kuteketea kwa moto.
Basi hilo Mbilinyi Express limeteketea kwa moto katika eneo la NONGANONGA lililopo katika barabara ya SONGEA NAMTUMBO majira ya saa saba za Mchana hii leo (30.07.2009)
Mkuu wa kikosi cha Zimamoto katika wilaya ya SONGEA KELVIN MAPUNDA amesema abiria wote waliokuwamo ndani ya basi hilo walifanikiwa kujiokoa kwa kutoka nje mara baada ya basi hilo kuwaka moto isipokuwa bibi mmoja aitwaye MWANANURU HASSAN ambaye ameumia kutokana na kukanyagwa na abiria wenzake.
Hata hivyo MAPUNDA amekiri kuwa kikosi chake kilichotumia mitungi ya kuzima moto badala ya gari la Zimamoto ambalo ni bovu, hakikufanikiwa kunusuru mali yoyote
No comments:
Post a Comment