Mwenyekiti wa chama mpira wa kikapu simon msofe alipokuwa akizungumza na waandishi hii kuhusu Bonanza la kwa shule za msingi
Basketball Dar es salaam wakishirikiana na Ali Hassan Mwinyi Elite School imeandaa bonanza kwa shule za msingi ambalo litaambatana na uzinduzi wa ligi ya Shule za Secondari Mkoa wa Dar es salaam siku ya Jumamosi tarehe 15/08/2009.
Bonanza hilo kwa shule za msingi litakuwa na dhumuni la kuhamasisha watoto wa kike kushiriki katika mchezo wa Mpira wa Kikapu lakini pia kuandaa mazingira ya kuanza kwa ligi ya Mashule kwa shule za Msingi
Tayari tunayo ligi ya mashule kwa sekondari ambayo itaanza rasmi siku hiyo jioni katika viwanja vya Tanesco mkabala na ubalozi wa Marekani uwanja unao tumiwa na timu ya Pazi
Baadhi ya shule ambazo tayari zimethibitisha ni Ali Hassan Mwinyi,GoodSamaritan,JKT kids,Polisi kids,Donbosco kids,Chang’ombe United kids,Pazi kids,Aghakhan na nyingine nyingi
Kwa kuwa tunatambua katika mashule mengi ya msingi hakuna viwanja hivyo tumetoa nafasi kwa zile timu za watoto ambazo zipo katika kituo au clubs za Mkoa wa Dar es salaam kuweza kushiriki na kutoa hamasa ili mwakani tupate shule nyingi
Tunategemea kuwa na wanafunzi 360 watakao shiriki kama wachezaji lakini tutakuwa na wanafunzi wasiopungua 900 kama watazamaji
Ratiba itapangwa leo baada ya kukutana na walimu wa michezo kwa ajili ya kupitia kanuni za mashindano
Tunapenda kuwashukuru Kwanza Bottlers kwa kutupatia Maji,Tigo pamoja na Unilever ,diwani Kimbau kwa mchango wake pia tunaendelea kupokea chochote kutoka kwa wahisani
Tunaomba ndugu zetu waandishi wa habari mtusaidie kufanikisha shindano hili.
No comments:
Post a Comment