baadhi ya wanachama wa simba wakimsindikiza mwenyekiti wa simba wakati akitembelea jengo la simba
Siku moja baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa simba RAGE ametembelea klabuni hapo na kujionea majengo yalivyo pamoja na matatizo yaliyopo klabuni hapo.
RAGE amesema klabu ya SIMBA haina umeme na haijawahi kulipa kwa muda wa miaka kumi na tano na inadaiwa zaidi ya milioni tatu .
Lakini tayari amekwenda TANESCO na umeme umarudishwa katika klabu hiyo .
Katika hatua nyingine RAGE amesema amemuomba WAMBURA kufuta kesi zote mahakamani ili waweze kujenga umoja katika klabu ya simba
No comments:
Post a Comment