HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

14 May 2010

TAIFA CUP ROBO FAINALI

Mabingwa watetezi IIala, Arusha na Mwanza ni miongni mwa timu zilizofuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la taifa, ‘Kili Taifa Cup’ baada ya kumaliza mechi za kwenye vituo vyao zikiwa katika nafasi za kwanza. Mikoa mingine iliyojihakikishia kucheza robo fainali ni Temeke na Singida. Arusha Kutoka Arusha, Woinde Shizza anaripoti kuwa wenyeji Arusha walijihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo ya ‘Kili Taifa Cup’ baada ya kumaliza wa kwanza katika kituo chao, wakishinda mechi zote tatu na kufikisha pointi tisa. Walishinda 3-0 dhidi ya Manyara, 2-1 dhidi ya Mara na jana walishinda 3-1 dhidi ya Kilimanjaro. Mara pia walishinda 5-1 dhidi ya Manyara jana na kukamata nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi sita. Mtwara Ilala walioshinda mechi mbili za kwanza kwa magoli 2-1 dhidi ya Mtwara na idadi kama hiyo dhidi ya Lindi, jana walishikwa shati na kutoka sare ya 3-3 dhidi ya Ruvuma. Hata hivyo, sare hiyo iliwapeleka Ilala robo fainali baada ya kufikisha pointi saba na kuongoza katika kituo hicho, licha ya kwamba Lindi walimaliza michuano hiyo kwa kishindo jana baada ya kuwafunga Mtwara kwa magoli 6-1. Dodoma Kutoka katika kituo cha Dodoma, Somoe Ng'itu anaripoti kuwa timu ya mkoa wa Singida ilitinga robo fainali za michuano hiyo baada ya kushinda 3-2 dhidi ya wenyeji Dodoma na kufikisha pointi saba ambazo ziliwaweka juu kileleni, pointi mbili zaidi ya timu ya taifa ya vijana wa chini ya miaka 20 'Ngorongoro Heroes', ambao waliingia katika michuano hiyo kwa nia ya kusaka uzoefu. Awali, Singida waliwafunga Kigoma 1-0 na kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Singida huku Ngorongoro wakishinda 2-1 katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Kigoma, jana. Mwanza Jijini Mwanza, George Ramadhani anaripoti kuwa, Mwanza Heroes waliingia robo fainali baada ya kuwafunga majirani zao Shinyanga kwa magoli 2-0 na kuongoza katika kituo chao baada ya kufikisha pointi saba. Awali, Mwanza walitoka sare ya 2-2 dhidi ya Tabora na kuwashindilia Kagera 3-1. Tabora walimaliza katika nafasi ya pili, wakifikisha pointi tano baada ya kutoka sare pia ya 1-1 dhidi ya Shinyanga na kupata ushindi wa mezani jana baada ya wachezaj wa Kagera kugomea mechi kutokana na uongozi wa mkoa Kagera kushindwa kuwapatia posho zao. Tanga Katika kituo cha Tanga, Temeke walifuzu kwa hatua ya robo fainali baada ya kushinda kwa magoli 3-1 dhidi ya Morogoro jana na kufikisha pointi saba ambazo ziliwaweka kileleni, pointi tatu zaidi ya Pwani waliomaliza katika nafasi ya pili baada ya jana kushinda 1-0 dhidi ya wenyeji Tanga. Iringa Katika kituo cha Iringa, wenyeji Iringa ‘Ruaha Stars’ walifuzu baada ya kuwashindilia Rukwa kwa magoli 6-0 na kufikisha pointi saba na magoli 8. Kinondoni walitoka sare ya 0-0 dhidi ya Mbeya. Washindi sita katika kila kituo, wataungana na timu nyingine mbili zilizoshika nafasi ya pili na kupata matokeo bora zaidi kucheza robo fainali za michuano hiyo zitakazofanyika jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers