Baada ya Cliford Ndimbo kumaliza muda wake wa miezi mitatu katika klabu ya SIMBA na kuondoka katika kiti cha usemaji wa klabu hiyo ,sasa klabu ya SIMBA imemrejesha msemaji huyo kuendelea na kazi yake .Mwenyekiti wa SIMBA Ismail Aden Rage amesema kamati ya utendaji imekaa na kuamua kumrudisha Cliford Mario Ndimbo katika nafasi yake kwa muda wa miezi sita kwa uangalizi kama atafanya vizuri watampa mkataba zaidi, lakini akishindwa kufanya vizuri ndani ya miezi sita ataondolewa katika nafasi hiyo. . Kwa hisani ya www.janejohn5.blogspot.com
No comments:
Post a Comment