Katika mpango wake kabambe wa kupanua
wigo wa mabondia wa “Kiafrika, Mashariki
ya Kati na Ghuba ya Uajemi” kujitangaza katika tasnia ya ngumi za kulipwa,
Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA)
limezindua taji jipya.
Taji hilo linajulikana kama “Ubingwa wa IBF Afrika, Mashariki ya Kati na
Ghuba ya Uajemi” kwa kizungu ni “IBF
Africa, Middle East and Persian Gulf Title” au (IBF/AMEPG).
Mpamnano wa kwanza wa ubingwa huo
utafanyika katika jiji la Windhoek
nchini Namibia Septemba 1, 2012 kati ya “Mtanzania
Rajabu Maoja” na bingwa wa Namibia Gottlieb
Ndokosho!
Mpambano mwingine unategemewa
kufanyika katika jiji la Accra nchini
Ghana kati ya bondia Richard Commey
wa Ghana ambaye kwa sas aanajifua nchini Uingereza na bondia kutoka nchi ya Qatar ambayo iko katika Ghuba ya Uajemi.
Juhudi hizi za IBF/USBA zinakuja
wakati ambapo shirikisho hili limeanzisha programu ya “Utalii wa Michezo” na kuziteua Tanzania na Ghana kama nchi za mfano kwa kipindi cha miaka mitatu
(3).
Akizungumzia kuhusu taji hilo jipya Rais
wa “IBF/USBA katika bara la Afrika,
mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi” Mtanzania
Onesmo Ngowi alisema kuwa mabondia wa Kitanzania
wanatakiwa kuzichangamkia fursa hizi ili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya
kuweza kugombea mataji ya juu zaidi.
Ngowi alibainisha kuwa kwa sasa ni mabondia
wachache sana wa Tanzania ambao wana viwango vya juu ukilingamisha na mabondai wan
chi za Ghana, Namibia, Afrika ya Kusini, Uganda, Nigeria na Misri.
Aliahidi kuwapatia mabondia wa
kiatnzania nafasi za kugombea mataji haya kila panapotokea nafasi hizi.
No comments:
Post a Comment