Nahodha wa klabu ya arsenal ya Uingereza Robin Van Persie ambaye alitangaza wazi mwezi uliopita kuwa hatosaini kandarasi mpya kuitumikia timu hiyo amejiunga rasmi ya jana na wachezaji wenzake huko ujerumani ambapo timu inatarajia kucheza na Fc Koln mwishoni mwa juma hili
Mholanzi huyo ambaye amevutia klabu nyingi za ulaya kutaka saini ikiwamo Juventus ya italia Man city ya uingereza na Man utd baada ya kuweka wazi kuwazi kuwa akubaliani sana uendeshwaji klabu yenye maskani yake huko kaskazini mwa london ambapo july 4 mwaka alichapisha kwenye tovuti yake, huku arsena ikimaliza miaka saba bila taji na ikiachwa alama 19 nyuma ya timu za jiji la Manchester.
Katika mahojiano na mija ya toavuti kubwa barani ulaya Van persie ameonyesha kuvutiawa na wachezaji wapaya ambao tayari klabu hiyo imeshawasajiri mpaka sasa ambao alikuwa nao katika kiwanja cha kufanyia mazoezi cha London Colney wiki iliyopita Olivier Giroud , Lukas Podolski, na Santi Cazola watakuwemo kwenye kikosi cha arsenal siku ya jumapili katika uwanja wa RheinEnergieStadion, ambao tayari mpaka sasa wameshapata mafunzo kutoka kwa kocha wa timu hiyo Arsene Wenger mabapo wanatajiwa kuongeza kasi ya ushambuliaji .
No comments:
Post a Comment