Rais
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba
udhamini unachangia kwa asilimia 59 pato la soka ya Tanzania, wakati mapato ya milangoni
ni asilimia 29.
Tenga
alisema hayo, wakati akifunga kozi ya Utawala na Usimamizi ya Shirikisho la
Soka la Kimataifa (FIFA), kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre, Dar es Salaam.
“Lakini
kwa wenzetu, mechi moja tu inaingiza Sh. Bilioni 8 za Tanzania (mapato ya
milangoni), ona sisi ambavyo tuko nyuma, kwa kweli tuna kazi kubwa na ngumu
bado mbele yetu,”alisema Tenga.
Tenga
aliwaambia washiriki wa semina hiyo ni kazi ngumu mno kuongoza soka Tanzania
kutokana na mwamko mdogo na uelewa pia, hivyo akawataka washiriki wa kozi hiyo watumie
vema mafunzo waliyoyapata kuongoza mchezo huo kwa ufanisi.
Tenga
aliwashukuru FIFA kwa kozi hiyo ambayo ilianza Agosti 6, mwaka huu ikishirikisha
wadau mbalimbali wa soka nchini, wakiwemo viongozi wa vyama vvya mikoa na
wachezaji.
Kwa
upande wake, Mgeni rasmi katika kufunga kozi hiyo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro
Premeum Lager, George Kavishe, wadhamini wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars alisema anawashukuru FIFA kwa kozi hiyo, kwani inasaidia maendeleo ya soka
nchini.
“Sisi
kama wadhamini wakuu wa mchezo huu hapa nchini, tunaamini mafunzo haya yatasaidia
sana kuleta ufanisi katika mchezo wetu, kwa hiyo acha niseme nawashukuru na
kuwapongeza FIFA,”alisema Kavishe.
Mbali
na kudhamini Taifa Stars, Kilimanjaro Premium Lager, pia ni wadhamini wa klabu
kongwe nchini, Simba na Yanga.
Kwa
ujumla, washiriki wa kozi hiyo iliyoendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA Dk Henry Tandau
wa Tanzania, Sinca Kanyenvu kutoka Botswana na Barry Bukolo kutoka Namibia walikuwa
ni viongozi kutoka TFF, Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), vyama vya mikoa, klabu
za Ligi Kuu na viongozi wa soka ya wanawake.
Washiriki
wa kozi hiyo walikuwa ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani,
Rais wa ZFA Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi,
Blassy Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud
Mvella.
Wengine
ni Katibu Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai,
wenyeviti wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi),
Dodoma (Nassoro Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
Makatibu
wa vyama vya soka vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent
Majiri), Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya)
na Dodoma (Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.
Washiriki
wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday
Kayuni, Ofisa Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy
Kabwe, Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba, Ofisa Sheria wa TFF, Neema
Lucumay, Ofisa wa Soka ya Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Soka ya wanawake)
na Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.
No comments:
Post a Comment