HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

10 August 2012

AFRICAN LYON YAMTAMBULISHA PABLO VELEZ




Kocha mpya wa timu ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam,  inayoshiriki  Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Pablo Ignacio Velez,  kutoka Argentina, akizungumzi na waandishi wa habari jijini Da re Salaa leo mchana wakati wa utambulisho wake na mkataba wa kuifundisha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao  . Kocha huyo amesaini Kandarasi  ya  miaka miwili  na timu hiyo. Katikati ni Mkurugenzi wa ufundi , Charles Otieno (kushoto) ni Meneja Mkuu , Rahim Kangezi.

KOCHA mpya wa timu ya soka ya African Lyon, Pablo Ignacio Velez, amewasili nchini tayari kuanza kuinoa timu hiyo na kuomba apewe muda wa kukisuka upya kikosi hicho huku akiahidi mabadiliko zaidi ya soka kwenye timu hiyo.
Pablo raia wa Argentina amesema hayo leo baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia timu hiyo na kusisitiza lengo lake kubwa ni kuhakikisha vijana wanapewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na ndivyo itakavyokuwa Afrika Lyon.
Amesema  ndoto yake  kubwa ilikuwa kufundisha soka barani Afrika hivyo wakati umefika  sasa kufanya lile ambalo alikuwa akiliota kutimia
kazi ya aina yoyote lazima ipewe muda na mchezaji lazima atengenezwe hivyo watanzania wawe na subira kwa ajili ya kupata matunda mazuri ya vijana hapo baadae kutoka African Lyon.
Kocha huyo aliyewai kuzichezea timu za taifa za vijana chini ya miaka 17 na 20 za Argentina hakusita kusisitiza suala la nidhamu kwa wachezaji wa timu hiyo ya ndani na nje ya uwanja.
"Nidhamu ni muhimu kwa wachezaji wangu cha msingi tushirikiane katika kufanikisha hili kwa vijana kwani mchezaji anatakiwa kati ya miaka 18 na 19 awe ametengeneza jina kupitia soka ,"  alisema Pablo.
Naye Mmiliki wa African Lyon, Rahmu Kangezi alisema lengo la kumleta kocha huyo ni kuhakikisha timu hiyo inajongea mbele zaidi.
Kangezi alisema licha ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja lakini wanaweza kumtumia Pablo kwa kipindi kirefu kulingana na mfumo wa kuhakikisha wanaendeleza vijana katika timu yao.
"Pablo ni zaidi ya kocha, ana uwezo pia amecheza mpira pia ni kocha wa kwanza kutoka Argentina kuja Tanzania hivyo tunaimani timu yetu ya African Lyon itafika mbali zaidi kisoka," alisitiza Kangezi.
Pablo mwenye miaka 38 aliyechukua mikoba iliyoachwa na Jumanne Chale amewai kuifundisha  klabu ya Atletico Colo Colo De Chile (1998).
Klabu nyingine alizowahi kufundisha ni Atletico Calchin (2000), Atletico Belgrano De Cordoba (1997), Atletico River Plate (1993-1995).
Klabu nyingine ni Banco De Cordoba (1991 na 1997), Deportivo Lasallano (1992) Atletico Argentino Penarol kwa miaka minne na klabu nyingine nyingi za Hispania na Argentina.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers