Pichani Mbuyu Tiwte Liyekuwa beki wa kati wa APR ya Rwanda ambaye kwa sasa inasemekana amesaini timu mbili zote za Tanzania Simba na Yanga kwa mujibu wa Mseamaji wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga alipokuwa akihojiwa na moja ya Radio kubwa jiji Dar es salaam amesema kuwa mlinzi huyo amesaini kandarasi ya kuitumikia Klabu yao kwa miaka miwili na utaratibu huo ulifanyika Kigali nchini Rwanda lakini akaongeza kusema kama mchezaji anaruhusiwa kusaini timu mbili sawa lakini wanachofamu wao ni kuwa wameshamlipa pesa zake zote na kilichobakia Ni Mbuyu Twite kuanza kutumikia Kandarasi hiyo ya Miaka Mitatu.
Aidha Katibu mkuu wa klabu ya yanga Mwesiga Celestine katika mahojiano na Radio alionekana kama hataki kunyoosha maneneo lakini kwa mujibu alivyokuwa akijibu ilionekana dhahiri Mbuyu Amesaini kandarasi na Klabu hiyo aliulizwa kwa maana hiyo Mbuyu Twite amesaini yanga bado kutangaza alisema akhasante sana na simu ikakatwa
japokuwa alisisitiza kuwa klabu hiyo itatoa taarifa ndani ya masaa ishirini na nne.
Kwa upande mwingine huu ndio ubabaishaji wa simba na Yanga kwani huwa haipiti miaka miwili au moja lazima itokee balaa ya mcheza kusaini mkataba timu zote mbili na kuwa gumzo katika maskio ya wanasoka na wachezaji ambao wamekuwa wakiwang'ang'ani huwa si kitu uwanja. SIMBA NA YANGA ZINATAKIWA KUACHA UBABAISHAJI HUU.
No comments:
Post a Comment