Kozi ya Uongozi na
Utawala ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) itafanyika Msimbazi
Center jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 6-11 mwaka huu ikiwa na washiriki
30.
Washiriki wa kozi
hiyo itakayonedeshwa na wakufunzi kutoka FIFA ni viongozi kutoka TFF, Chama cha
Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, klabu za
Ligi Kuu na viongozi wa mpira wa miguu wa wanawake.
Walioteuliwa
kushiriki ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, Rais wa ZFA
Amani Makungu, wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Ahmed Mgoyi, Blassy
Kiondo, Stanley Lugenge, Khalid Abdallah, Hussein Mwamba na Eliud Mvella.
Wengine ni Katibu
Mkuu wa ZFA, Kassim Salum, Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai, wenyeviti wa
vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (Jamal Malinzi), Dodoma (Nassoro
Kipenzi) na Pascal Kihanga (Morogoro).
Makatibu wa vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa ya Mara (Mugisha Galibona), Mtwara (Vincent Majiri),
Morogoro (Hamisi Semka), Kagera (Salum Chama), Tanga (Beatrice Mgaya) na Dodoma
(Stuart Masima). Pia yumo Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Hilal na Makamu
Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga.
Washiriki wengine ni
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni, Ofisa
Habari, Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Masoko na Matukio, Jimmy Kabwe,
Mkurugenzi wa Mashindano, Saad Kawemba, Ofisa Sheria wa TFF, Neema Lucumay,
Ofisa wa Mpira wa Miguu wa Wanawake, Grace Buretha, Amina Karuma (Mpira wa
miguu wa wanawake) na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa.
No comments:
Post a Comment