Angetile Osia Katibu mkuu TFF |
Katibu mkuuu wa shirikisho la mpira
wa miguu Tanzania ,Angetile Osia amethibitisha kuwa viongozi wa fc Lupopo ya jamhuri ya
kidemokrasia ya kongo wamekutana na viongozi wa simba katika makao makuuu ya
shirikisho hilo kujadiri marejesho ya fedha za mchezaji Mbuyu Twite aliyehamia
klabu ya yanga, mwanzo viongozi hao walitaka kukabidhi pesa kwa viongozi wa tff
ambapo waliongea kwa simu na katibu mkuu wa tff angetile ambaye aliwatolea nje
kupokea pesa zao
“ Angetile anasema kuwa walimpigia simu
ili wakabidhi pesa hizo kwake yeye lakini akawatolea nje kwa kuwaambia kuwa
hawezi kupokea pesa hizo kwani sio za
tff “ baada ya kuwaambia walikata simu lakini baadae walimpigia tena kuwa
wameongea na viongozi wa klabu ya soka ya simba wakutane katika shirikisho la
soka la Tanzania tff iliwaje warejeshe pesa, Osia anasema kuwa aliwakubalia waje
watumie ofisi za tff kwa makabidhiano yao lakini tff na walizungumza lakini tff haikuwemo kwenye kikao na hawajui walichozungumza 'tff ,haitahusika katika makabidhiano hayo kwani wao hawahusiki
na shughuri za usajiri wa mchezo huo mazungumzo hayo ni baina ya klabu husika
na mchezaji huyo.
Kwa upande mwingine amesema kuwa
katika zoezi la usajiri kuna timu nyingi zitakuja kuumia kwani zimecheza faulo
nyingi katika zoezi hizo na vilevile akafafanua kuhusu utaratibu wa usairi na
kusema kuwa mchezaji ambaye ana mkataba na timu yake anapotakiwa na timu
nyingine lazima klabu izungumze na klabu nyenzake lakini kama mchezaji atakuwa
yupo huru 'klabu inaweza kuzungumza na mchezaji husika kwasasa kamati ya Alex
mgongolwa itakapokutana haitaziona aibu timu zilizo fanya kinyume na
utaratibu.
No comments:
Post a Comment