Mchezazji wa zamani wa timu ya taifa ya tanzania, Renatus
Njohole ambaye pia aliwahi kucheza mpira nje ya Tanzania kupitia Taasisi yake
Ya Njohoke Foundation' Leo watacheza mechi katika uwanja karume mara baada ya
kushindwa kufanikiwa kupata uwanja wa taifa Akizungumza kwa masikito Moja kati ya walatibu wa mechi hiyo Jamhuri
Kiwelu Ambaye akutakata kuzungumzia swala hilo kwa wakati huo alihituhumu wazi wazi
wizara ya habari utamaduni na michezo kuwa ndiyo imekuwa Mstari mbele kurudisha
maendeleo ya michezo nyuma kwa Tanzania baada kuwekewa masharti magumu
Aidha akasema Leo majira ya saa kumi kamili katika uwanja
wa karume Timu ya Njohole 11 Itapambana
na wachezaji waliocheza soka miaka ya nyuma aidha dhima kubwa ya mchezo huo ni kuwaleta wachezaji wa zamani na
taasisi hiyo na kuwasidia wachezaji wa zamani ambao walilitea sifa taifa hili lakini
kwa bahati mbaya wamesahaulika amesema Elikyembe Boniface ambaye ni Kiongozi wa kampuni hiyo.
Jamhuri kiwelu amesema wachezaji wazamani watakaocheza mechi
ni waliocheza mpira zamani na wale sasa wanaotoka katika familia za soka lengo
ni kuwaleta pamoja wachezaji wa soka hasa wa zamani ambao walileta heshima
katika taifa hili katika hatua mbalimbali lakini wamesahaulika na serikali.
Taasisi hii itawasaidia kwa namna moja au nyingine ikiwemo kuandika historia
zao.
No comments:
Post a Comment