Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za
kifo cha mwamuzi wa zamani wa kimataifa Msafiri Mkeremi kilichotokea leo
alfajiri (Agosti 2 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Wilaya ya Urambo
mkoani Tabora.
Licha
ya kuwa mwamuzi, Mkeremi aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) sasa TFF kwa vipindi viwili
tofauti. Pia aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha
Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT). Vilevile
aliwahi kuwa mkufunzi wa waamuzi, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na
Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) Mkoa
wa Pwani Kwa
upande wa vyama vya mpira wa miguu aliwahi kuwa kiongozi katika mikoa
ya Tabora, Pwani na wilayani Mpanda katika Mkoa wa Rukwa. Msiba
wa Mkeremi uko nyumbani kwake Urambo, na kwa mujibu wa mtoto wake
Masoud Mkeremi, atazikwa Jumamosi kwenye makaburi ya Msafa yaliyoko
wilayani Urambo. TFF
inatoa pole kwa familia na kuitaka kuwa na uvumilivu katika kipindi
hiki kigumu. Pia TFF itatoa ubani wa sh. 200,000 kwa familia ya marehemu
kama rambirambi zake. Marehemu aliyekuwa akisumbuliwa na presha na ugonjwa wa kisukari ameacha wajane wawili na watoto 12. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amina
No comments:
Post a Comment