Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) limeandaa semina kwa ajili ya makamishna (match commissioners),
watathmini wa waamuzi (referees assessors) na waamuzi wa daraja la kwanza
(class one) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Ligi Kuu inayotarajia kuanza
baadaye mwezi ujao.
Kwa upande wa makamishna na
watathmini wa waamuzi, semina itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti
29-30 mwaka huu. Washiriki wanatakiwa kujigharamia kwa kila kitu; usafiri,
malazi na chakula wawapo kwenye semina.
Semina kwa waamuzi itafanyika katika
vituo vya Dar es Salaam na Mwanza kuanzia Agosti 31- Septemba 2 mwaka huu. Pia
nao watajigharamia kwa kila tu. Waamuzi watakaoshiriki semina hiyo ni ambao
hawakushiriki ile iliyofanyika Juni mwaka huu na wale walioshiriki lakini
hawakufaulu mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test).
Waamuzi wenye beji za Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) hawashiriki kwa vile wao wamekukuwa
wakishiriki semina zao zinazoandaliwa na FIFA kila baada ya miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment