timu hiyo ililazimishwa sare ya
1-1 na Jamhuri ya Zanzibar katiaka mechi ya kwanza , magoli ya simba yalifungwa na
Christopher Edward dakika ya 11 na 26 kwa penalti.
Mtende ilimaliza mechi hiyo pungufu mechi hiyo, baada ya Rajab Mzee kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa
kumtolea lugha chafu refa wa kike, Judith Gamba.
Simba
inatumia kikosi chake cha pili kwenye mashindano haya, ambacho kipo
chini ya kocha Suleiman Abdallah Matola, Nahodha wa zamani wa Simba SC.
Katika mechi nyingine iliyofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi,
wenyeji Azam wamefungwa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Magoli ya Mtibwa yalipatikana kipindi cha pili,
wafungaji ni Shaaban Kisiga na Hussein Javu.
Mtibwa iliifunga Polisi Moro 2-0 kwenye mchezo wa kwanza, sasa
inaongoza kundi hilo kwa Alama sita, ikifuatiwa na Azam yenye Alama
tatu, ambayo katika mechi ya kwanza, iliifunga Super Falcon 2-0.
No comments:
Post a Comment