Semenya alitimka kwa kasi dakika za mwisho lakini hakuweza kumpita mwanariadha wa Urusi |
Caster Semenya aliikosa medali ya dhahabu katika mbio
za mita 800 siku ya Jumamosi mjini London, baada ya kushindwa na Mrusi
Mariya Savinova, ambaye alijiongezea medali zaidi, akiwa tayari ndiye
bingwa wa mashindano ya riadha ya dunia.
Semenya, mwanariadha mwenye umri wa miaka 21
kutoka Afrika Kusini, na ambaye alifuzu kuingia fainali kwa kuandikisha
muda wa kasi zaidi, alijaribu kutimka kwa kasi ya juu sana katika hatua
chache za mwisho, lakini akawa tayari amechelewa kumpita Savinova, na
ilimbidi aridhike na medali ya fedha kwa kumaliza katika nafasi ya pili.Inaelekea hali ya ushindani wa Semenya imekuwa mara nzuri, mara mbaya, tangu shirikisho la riadha ulimwenguni, IAAF, kumsitisha asishiriki katika mashindano ya riadha, na huku likifanya uchunguzi wa jinsia, tangu alipoibuka bingwa wa mashindano ya riadha ya dunia mwaka 2009.
Bingwa mtetezi kutoka Kenya, Pamela Jelimo, hakuwa na lake katika mashindano hayo ya Jumamosi, kwani alimaliza katika nafasi ya nne, na alipitwa hatua za mwisho na Mrusi Ekaterina Poistogova, ambaye aliondoka na medali ya shaba kwa kumaliza katika nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment