Wachezaji
hao wamechaguliwa na jopo la makocha kwa shirikiana na wataalam wengine
kutoka shirikisho la soka Tanzania (TFF)
na chama cha mpira wa miguu mkoa Dar es Saalam (DRFA) uchaguzi ambao
ulifanyika wakati wa fainali ya michezo ya kuibua vipaji ya Airtel
Rising Stars zilizofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini
Dar es
Salaam mwezi Juni.
Michezo hiyo ilishirikisha timu kutoka mikoa ya Lindi, Mbeya, Arusha,
Ilala, Temeke na Kinondoni.
Akiongea
na waandishi wa habari katika ofisi za TFF leo, afisa Maendeleo wa mpira wa
miguu nchini Salum Madadi aliwataja vijana watakaowakilisha Tanzania kuwa ni
Denis Richard, Juma Hamza, Abdul Selemani, Ishaka Shekolowa na Bakari Ally
kutoka mkoa wa kisoka wa Temeke.
Wengine
ni Abdulatif Mohamed, George Joseph na Badilu Said (Lindi), Said Kassim, Amos
Ikungula, Paul Balama na Goodluck Mabiku (Ilala), Joel Kasimula na Ibrahim
Mtenga (Mbeya), Sntkony Angelo na Suleiman Yunus (Arusha).
Mashindano
hayo yanayotajiwa kuwa na ushindani mkali yatashirikisha wachezaji wengine
nyota wa ARS kutoka nchi za Kenya,
Uganda, Malawi, DRC, Congo Brazzaville, Nigeria, Ghana, Zambia, Niger, Gabon,
Burkina Fasso, Sierra Leone, Chad, Madagascar na Tanzania.
Mkurugenzi
wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya amesema kuwa lengo la
mashindano hayo ya kimataifa ni kuwapa vijana fursa zaidi ya kuendeleza vipaji
vyao na kupata uzoefu.
“Hii ni nafasi kwa wanasoka hawa chipukizi
kuweza kupanua jiografia yao na kujenga urafiki na vijana wenzao kutoka nchi
mbali mbali”
Michuano
hiyo itafuatiwa na kliniki ya soka ya kimataifa ambayo pia itafanyika Nairobi
chini ya walimu wa soka la vijana kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester
United ya Uingereza.
Kliniki kama hii ilifanyika mwaka jana kwenye uwanja wa
kisasa wa soka jijini Dar es Salaam na kushirikisha vijana kutoka Kenya,
Malawi, Sierra Leone na wenyeji Tanzania.
Katika
kliniki ya mwaka huu, Tanzania itawakilishwa na wachezaji sita miongoni mwao ni
wavulana watatu na wasichana watatu ambao waliibuka kuwa wachezaji bora wakati
wa fainali za Taifa jijini Dar es Salaam mwezi Juni.
Airtel
Rising Stars ni mpango kabambe wa kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka wanaochipukia
barani Afrika. Walengwa ni wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi
na saba ambao watapata fursa ya pekee ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya waatalum
wa mpira wa miguu wa kitaifa na kimataifa.
No comments:
Post a Comment