Mzozo katika chama ulizidi wiki iliyopita, wakati
waziri wa michezo, Paul Kamara, aliilaumu bodi ya SLFA kwa uzembe, na
akaivunjilia mbali.
Lakini ilipofahamika kwamba shirikisho la FIFA
lilikuwa likiangalia hali iko vipi, na kulikuwa na uwezo wa kuipiga timu
ya Sierra Leone marufuku isicheze katika mechi za kimataifa, rais
Ernest Bai Koroma aliamuru bodi ya SLFA irudishwe kazini.
Kufuatia hayo, FIFA ilisitisha uchaguzi uliokuwa
ufanyike mwishoni mwa wiki, na ikamtuma Corvaro katika taifa hilo la
Afrika Magharibi, kuzungumza na wahusika wote.
Kulingana na Corvaro, kuna "hali ya watu waliopo
katika Kamati ya Rufaa ambao hawana uhalali wowote katika kuwa hapo,
maanake hawakuidhinishwa vyema, na tayari wameamua kauli fulani
kuhusiana na utaratibu wa uchaguzi."
No comments:
Post a Comment