HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

21 September 2012

NDONDI TAIFA , KUFEHEDHESHANA KUUMIA KOTE MALIPO Sh. 10,000



Maandalizi mabovu pamoja na ukata vimeathiri mashindano ya Taifa ya Ngumi za Ridhaa ambayo yameshuhudia washindi wa watatu wa juu wa taifa wakizawadiwa kati ya Sh. 30,000 na Sh.10,000 na vyeti vya ushiriki bila ya medali huku waandaaji Shirikisho la Ngumi (BFT) wakisema waliopewa tenda ya kuchonga medali wamechelewa kumaliza kazi hiyo.

Mabingwa wa Taifa katika uzani mbalimbali, ambao medali zao sasa watakabidhiwa siku zijazo zitakapomalizika kuchongwa, waliondoka na Sh. 30,000 kila mmoja huku washindi wa pili wakipata Sh. 20,000 na watatu Sh.10,000.


Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, alisema kuwa mtu aliyepewa kazi ya kuchonga medali alikuwa hajamaliza kazi hiyo badala yake akawasilisha Sh. 250,000 ambazo walizitumia kutengeneza vyeti kwa ajili ya washiriki wote. 


Bondia Said Hofu wa JKT alitwaa ubingwa wa taifa uzani wa Fly kg. 49 baada ya kumdunda Maulid Athuman wa Polisi kwa pointi za majaji 5-0 katika fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam jana jioni.


Huku akishangiliwa na mamia ya mashabiki, Hofu alionyesha dhamira ya kutwaa ubingwa tangu raundi ya kwanza kutokana na 'kumnyeshea' mpinzani wake 'mvua ya makonde' mfululizo.


Kwa ushindi huo, Hofu aliizawadiwa Sh. 30,000 na cheti huku akielezwa kuwa medali yake ya dhahabu itafuata siku zijazo, wakati huku mpinzani wake anayetarajiwa kupata medali ya fedha, aliondoka na zawadi ya pesa taslimu Sh. 20,000. Marko James na Hafidh Bamtulah ambao walistahili medali ya fedha waliondoka na Sh. 10,000 kila mmoja.


Pambano lingine lilikuwa kati ya Yahaya Malik wa Polisi aliyekung'utwa na Sunday Elias wa Pwani kabla ya kuokolewa na mwamuzi katika fainali ya uzani wa light fly kg. 52 na bingwa kujinyakulia Sh. 30,000 huku wa pili akiondoka na medali ya fedha Sh. 20,000.


Kwa upande wa wanawake, Mather George wa Kilimanjaro aliibuka kinara kwenye fainali ya uzito wa Fly baada ya kumpiga Irene Kimaro wa Tabora kwa pointi za majaji 5-0. Kwa ushindi huo Mather alizawadiwa Sh. 30,000 na majani ya chai ya Tausi wakati mpinzani wake akiondoka na majani kama hayo na Sh. 20,000 huku Mariam Andrew akikosa mpinzani katika fainali hiyo.


Akizungumza wakati wa kufunga mgeni rasmi kwenye mashindano hayo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo (BMT), Henry Lihaya aliwapongeza mabondia wote kwa kushiriki mashindano hayo na kuwataka wale watakaoteuliwa kwenye timu ya taifa kujifua zaidi ili kuliwakilisha vema taifa.


Michuano hiyo ina lengo la kupata timu ya taifa itakayoiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Afrika yatakayofanyika baadae Oktoba jijini Cassablanca, Morocco
.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers