Timu ya mchezo wa vishale (darts) ya
Lugalo Kombaini ambayo inamilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
kambi ya Lugalo, juzi ilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa mchezo huo mkoa
wa Dar es salaam.
Katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo huo nchini, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yao ya Safari Lager na kufanyikia kwenye ukumbi wa Urafiki, Kombaini walitwaa ubingwa huo baada ya kujikusanyia pointi 18 katika michezo yake yote.
Lugalo kwa kutwaa ubingwa huo ilizawadiwa fedha taslim Sh.200,000 pamoja na kikombe cha ubingwa.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na Upanga ambao walipata pointi 16 na kujinyakulia fedha taslim Sh.150,000 na kikombe na waliokuwa mabingwa watetezi, Polisi Barracks walishika nafasi ya tatu baada ya kupata pointi 13 na kuondoka na Sh.75,000 na kikombe.
Mashindano hayo yalishirikisha klabu 10. Nyingine ni Friends (10), Magereza (8), Mbezi (7), Kashundu (6), Ibukoni (5), Kawe (4) na Kimanga (3).
Kwa upande wa wanawake, klabu ya Kimanga ilitwaa ubingwa huo na kuzawadiwa Sh.50,000, Lugalo ilishika nafasi ya pili na kupewa Sh.30,000, wakati Polisi Barracks iliambulia Sh.20,000 kutokana na kumaliza ikiwa nafasi ya tatu.
Pia timu zote zilizoshiriki mashindano hayo kila moja ilipewa Sh.80,000 na cheti ikiwa kama motisha kwa ushiriki wao.
Zawadi zote hizo zilikabidhiwa na aliyekuwa mgeni rasmi ambaye ni meneja mauzo wa kampuni ya TBL katika wilaya za Kinondoni na Ilala, Victor Kavishe.

No comments:
Post a Comment