Kocha wa timu ya taifa ya mpira wa
pete ya Tanzania Marry Protas amekuwa katika wakati mgumu katika kuchagua
wachezaji watakao jiunga na timu ya Tanzania baada ya wachezaji hao kuonyesha
uwezo wa hari ya juu katika mashindano yanayondelea huko mkoani mbeya
Kocha huyo ameshangazwa na viwango
vinavyooneeshwa na amekiri kuwa katika wakati mgumu kuchagua wachezaji katika timu ya
taifa
Kaimu katibu mkuu wa Chama cha mpira
wa pete Tanzania Rose Mkisi, Amesema
mashindano hayo yameibua vipaji vya hari ya juu.ambapo yananyika katika uwanja
wa sokoine jijini Mbeya ambapo jumamatatu yatafika Tamati
Mkisi pia ameipongeza JKT Ruvu na
shule ya Sekondari ya Filbert Bayi kuwa
ni timu zilizoonesha vipaji na kuwapa wachezaji wadogo nafasi ya kucheza
na kuonyesha uwezo mkubwa aidha alikanusha kuwa hakuna mwamuzi au timu yoyote
inayopendelewa “ Mkisi alikataa kutoa
maoni kuhusu madai kuwa wanapendelea
hasa waamuzi wa kigeni “wanachokifanya
wasimamizi hawa sio kazi yako. Hutakiwi kufahamu lolote kuhusu wakufunzi hawa
kutoka Malawi kama unataka habari ,unaweza kuandika kuhusu mashindano alisem
mkisi kabla hakata ya simu hewani
Shirikisho la mpira wa pete la dunia
IFNA katika taarifa yake ya mwisho katika tovuti yao lilisema chaneta imeakodi
wasimamizi kutoka Malawi Ellenour Ndekhatani Mapulanga na Rebecca Kawanga
Dulanya kusimamia mashindano hayo
“Hongera kwa wakufunzi hawa
kutoka Malawi Ellenour Ndekhatani Mapulanga na Rebecca
Kawanga-Dulanya ambao wamearikwa kusimamia
michuano hiyo mikubwa kwa Tanzania “
Dulanya alichaguliwa baada ya uwezo
mkubwa na kuwavutia watanzania katika mashindano ya klabu bingwa ya Africa yaliyoyafanyika takriban miezi mine iliyiyopita
Kitambo kifupi , Mapulanga, ambaye mlinzi wa
zamani wa Malawi Queens , alitupiwa
jicho zaidi baada ya kupigiwa kura kuwa msimamizi bora katika taarifa za kila
wiki za IFNA
No comments:
Post a Comment