Andy Murray, hatimaye amefanikiwa kuondoa mkosi wa
Uingereza wa kungoja kwa kipindi cha miaka 76 kunyakua ubingwa wa
mashindano makuu ya Tennis ya Grand Slam kwa wanaume alipomshinda Novak
Djokovic katika fainali ya mashindano ya Marekani. Muingereza wa mwisho
kutwaa taji hilo alikuwa Fred Perry mnamo mwaka 1936.
Murray,mwenye umri wa miaka 25, alishinda kwa
seti tatu kwa mbili, 7-6 (12-10) 7-5 2-6 3-6 6-2 katika kipindi cha saa 4
na dakika 54 katika uwanja wa Arthur Ashe mjini New York.
Katika kipindi cha miezi michache iliyopita
Murray pia alifanikiwa kufika fainali ya mashindano ya Wimbledon na pia
kushinda nishani ya dhahabu katika michuano ya Olympiki mjini London.
"Nilipotanabahi kwamba nimeshinda ,nilipigwa na
mshtuko kidogo. Nilipumua kweli lakini nilijawa na hisia nzito",
aliongeza Murray.
Licha ya mafanikio yake mengine,hapana shaka
kwamba matokeo haya, yatakuwa na athari kubwa zaidi kwa mchezo wake
binafasi na mustakhabali wa tennis nchini Uingereza.
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment