Steven George Lutego ni kijana mdogo
mwenye umri wa miaka 16 mwanafunzi wa kidato cha kwanza, mkazi wa
Kurasini jijini Dar es Salaam mwenye dhamira ya kuiletea sifa Tanzania
kwa kuleta medali ya dhahabu katika michezo ya Olympic ya Rio de janeiro
nchini brazil Brazil mwaka 2016.
Dhamira ya Steven imejengwa na
inaendelea kujengwa na baba yake George Lutego ambaye hapo zamani
alikuwa ni mchezaji wa ngumi lakini hakuwa na sifa kubwa ya kuliletea
Taifa hili lenye wingi wa vipaji ambavyo havichimbwi wala kutafutwa kama
inavyotafutwa dhahabu na mafuta aridhini.
Akiongea na Rockersports Steven amesema
amekuwa kila siku akipewa risala na baba yake George kuwa anataka
kumuona akifanya mazoezi ya ngumi kila siku jioni isipokuwa jumapili tu
kwa kuwa baba yake huyo anataka kuiona medali ya dhahabu mwaka 2016
iliwa imeletwa na mtoto wake.
Amesema baba yake amemnunulia vifaa
vyote vya mchezo wa ngumi ikiwa ni pamoja na kumtengenezea ka-gym kadogo
kwa ajili ya mazoezi yake lakini pia amekuwa amkienda katika viwanja
vya wazi kufanya mazoezi yake.
Steven anasema baada ya kukubaliana na
baba yake tayari amekuwa katika mazoezi ambayo imejengeka akilini mwake
kiasi hata akiwa shuleni amekuwa anafikiria ndoto hiyo ya kwenda Brazil
kuleta Medali.
Anamshukuru baba yake mzazi kwa kuona
kipaji chaken cha ngumi sasa amemtafutia kocha ambaye ni mdogo wake
Frank Lutego ambaye ni ambaye kila siku anachoma mafuta kutoka Gongo la
Mboto kumfuata Steven uwanja wa taifa kumpa mazoezi.
Steven ana umri wa miaka 16, na mpaka
Olympic ya Brazil itakapokuwa imefika ni wazi atakuwa ana umri wa miaka
20 umri ambao haswa ndio muafaka kwa kijana kutakata katika medali ya
michezo.
Baba yake na Steven ambaye ni mwana
michezo mzuri anafanya mazoezi ya ngumi kujiweka fiti katika mwili wake
ameongea na Rockersports akisema yuko tayari kumpatia Steve kila kitu
kinacho husu maandalizi yake kama alivyo anza ili kufanikisha ndoto yake
yeye kama baba lakini sifa kwa kijana wake ambaye tayari ameanza
kuonyesha mwelekeo mzuri katika mchezo huo.
Mdau mwingine ni wewe msomaji wangu,
kama kuna kijana karibu yako awe mtoto wako, mtoto wa kaka, mtoto wa
mjomba mtoto wa jirani vyovyote vile mwenye umri kama huo au unaofanana
na huo yaani kuanzia miaka 13, 14, 15 na kuendelea na umegundua kuwa ana
kipaji jaribu kumuweka wazi kwa kile alicho nacho na sema unakipaji cha
aina fulani ili ajitambue ili awe na moyo.
Wasiliana na vyama vya michezo husika na
eleza unacho kiona ili kuokoa kipaji chake huenda ata utajiri mkubwa
ndani yake lakini hajitambui. Baba yake Steven, Geroge Lutego amekiona
kipaji cha mwanae na anakiendeleza na wewe fanya sasa.
No comments:
Post a Comment