Timu
yetu ya taifa ya vijana wa umri wa chini ya miaka kumi na saba (U.17)
Serengeti Boys, wameondoka leo asubuhi kwenda mkoani Mbeya kuendelea na
maandalizi ya kufuzu fainali za vijana zitazofanyika nchini Morocco
mwaka 2013. Timu yetu imepangiwa kupambana na timu ya taifa ya vijana wa
Misri (Egypt) katika hatua inayofuata, pambano hilo linatarajia
kufanyika Oktoba 2012. Timu yetu ilipata ushindi baada ya timu ya vijana
ya Kenya kujitoa kwenye michuano hii.
Timu
imekwenda mkoani Mbeya kwa mwaliko wa Chama cha Mpira wa Miguu cha
Wilaya ya Mbeya Mjini (MUFA), ikiwa huko chama hicho kitaihudumia kwa
malazi, chakula na huduma nyingine ndogondogo. Timu inategemea kupangiwa
michezo kadhaa ya majaribio na timu kabambe za mkoani humo ikiwemo
Mbeya City, Tanzania Prisons na timu za kombaini.
Shirikisho la Mpira
wa Miguu nchini linapenda kutumia fursa hii kuishukuru na kuipongeza
MUFA, kwa kuonyesha mfano unaostahili kuigwa na wadau wengine, wa
kushirikiana katika maandalizi ya kuziandaa timu zetu za taifa. Kitendo
hicho kinaonyesha kuguswa, uwajibikaji, uzalendo na ukomavu katika
kutatua matatizo kwa vitendo na sio kwa lawama bila suluhisho.
Shirikisho
pia linaishukuru benki ya NMB kwa kutoa msaada wa jezi seti moja na
fedha sh. Millioni tano, zilizowezesha vijana hawa kupata posho zao za
kambi na kusafiri kwenda Mbeya. Itakumbukwa kuwa benki ya NMB imekuwa na
mchango mkubwa sana katika maendeleo ya soka ya vijana kwa muda mrefu
sasa. Kwa kipindi cha miaka sita (2006-2010) iliyopita ilidhamini
mafunzo ya makocha wanaojihusisha na program za maendeleo ya vijana
nchini, vilevile ilitoa mipira ya program za vijana kwa vyama vya mikoa.
Hivyo tunaishukuru kwa kuthamini mchango wao huo na kwa kuendelea kutoa
msaada ili kuhahakisha inalinda mafanikio ya program hizo.
Shirikisho
linapenda kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia kuwaandaa vijana
wetu hawa pekee waliobaki kwenye mashindano. Mafanikio ya timu yetu ya
taifa (Taifa Stars) siku za usoni yanategemea sana msingi bora wa vijana
hawa. Hivyo ni vema tukashirikiana kama walivyojitokeza MUFA na NMB.
Hutisiti
kueleza bayana kuwa kama si wadau hawa kambi ya vijana ilikuwa
inavunjika, na baada ya kurudi Mbeya kama hakutakuwa na wadau wengine
watakaojitokeza basi uwezo wa kuendelea na kambi ya maandalizi kwa
vijana wetu utakuwa finyu mno.
Shirikisho
lina imani kuwa wakazi wa Mbeya watatoa ushirikiano wa hali ya juu
wakiongozwa na Chama cha Mpira cha Mkoa (MREFA), kwa Serengeti Boys ili
kufanikisha maandalizi hayo.
No comments:
Post a Comment