Rais wa shirikisho la soka nchini
TFF Leordinga Tenga amewataka waamuzi wa mpira wa miguu barani Afrika
kufuata kutafsiri vizuri sheria za mpira wa miguu ili kuleta maendeleo
ya mchezo huo barani humu.
Kauli hiyo ameitoa hii katika hotuba yake ya ufunguzi wa kozi
ya wakufunzi wa waamuzi (Futuro III Refereeing Course) ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambayo imeanza leo katika hotel ya Holiday inn jijini Dar es Salaam.
Jumla
ya washiriki katika kozi hiyo itakayoanza saa 3 asubuhi kwenye hoteli
ya Holiday Inn ambao wanatoka katika nchi 21 za Afrika ni 69. Kozi hiyo
inayotarajiwa kumalizika Septemba 22 mwaka huu inafanyika katika maeneo
mawili ya ufundi (technical) na utimamu wa mwili (fitness).
Nchi
washiriki ni Afrika Kusini, Botswana, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Ghana,
Kenya, Lesotho, Liberia, Malawi, Mauritius, Namibia, Nigeria,
Seychelles, Sierra Leone, Somalia, Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia
na Zimbabwe.
Washiriki
kutoka Tanzania kwenye kozi hiyo ni Joan Minja, Leslie Liunda na Soud
Abdi (technical) na Riziki Majalla (fitness).
Baadhi
ya wakufunzi wa kozi hiyo wanaotoka FIFA na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) ni Carlos Henriques anatoka Afrika Kusini, Fernando
Gracia (Hispania), Steve Bennett (Uingereza), Tarek Bouchamaoui
(Tunisia), James Sekajugo (Uganda), Bester Kalombo (Malawi), Felix
Tangawarima (Zimbabwe) na An-Yan Lim Kee Chong (Mauritius).
Tenga ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Baraza la Vyama vya
Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya CAF na mjumbe wa Kamati ya Vyama (Associations Committee) ya
FIFA amesema ni vizuri mafunzo hayo yakatumiwa vizuri sio tu kutoa
elimu kwa waamuzi juu ya mabadiliko katika sheria za soka bali pia ni
kuleta mtazamo mpya katika tasnia ya waamuzi ulimwenguni.
ROCKERSPORTS UNDSTAND
No comments:
Post a Comment