HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

4 September 2012

Waziri amrejesha kazini Katibu ZFA


Aliyekuwa Katibu  Mkuu wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Kassim Haji Salum, amerejeshwa kazini mara moja, siku kadhaa baada ya kusimamishwa na uongozi wa chama hicho kwa madai mbalimbali. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk, mbele ya viongozi wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) na watendaji wengine wa wizara yake,Waziri huyo amesema  kuwa hatambui uamuzi wa ZFA kumsimamisha kazi Katibu huyo, akisema umekiuka mamlaka aliyopewa kama Waziri, kuteua Katibu baada ya kushauriana na uongozi wa juu wa chama hicho.katibu huyo alifukuzwa kazi kwa madai ya kutokujua baadhi ya mambo ya komputa na hivyo ZDFA kumpiga chini.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers