Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la mpira wa Miguu Duniani FIFA, limeongeza adhabu kwa mchezaji wa timu ya taifa ya Nicaragua baada ya chama cha soka cha nchi hiyo kumfungia maisha kucheza soka lakini fifa imempiga marufuku mchezaji huyo kutokujihusisha na Shughuri zozote zinahusu Mchezo wa soka kwa ni katika ulimwengu wa kimataifa kitendo hicho hakiruhusiwi kabisa .
Armando Jose Collado Lanuza alijuhusisha na upangaji wa matokeo katika mechi ya kirafiki dhidi Guatemala mchezo uliochezwa Sept mwaka 2010 katika jiji la Miami.
Baada ya kumalizika kwa uchunguzi uliofanywa na chama cha nchi husika, iligundulika mchezaji huyo alihusika katika kupanga matokeo ambapo mchezo huo ulichezwa katika jiji la Miami
Maamuzi ya fifa yalichukuliwa mara baada ya kupitia stakabadhi katika jalada la mashtaka hayo na kwa mijibu wa kifungu cha 136 katika kanuni za fifa sasa atakuwa haruhusiwi kabisa kujihusisha na soka na shughuri zozote zile zihusuzo mchezo wa soka .

No comments:
Post a Comment