HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

9 October 2012

Papa Diop aingia Birmingham City



Birmingham City imesaini mkataba wa muda mfupi na mchezaji Papa Bouba Diop.
Baada ya kufanya mazoezi na timu ya Chelsea kwa wiki kadhaa zilizopita, mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal mwenye umri wa miaka 34 amefaulu katika vipimo vya afya na atatia saini mkataba wa mwezi mmoja, wakati maombi ya visa yake yakisubiriwa.Diop alijenga jina lake katika soka la England baada ya kujiunga na Fulham akitokea timu ya Lens ya Ufaransa mwaka 2004.
Aliichezea timu hiyo kwa misimu mitatu akiwa na Fulham, ambako alicheza pamoja na boss wa Chelsea, Lee Clark.
Baada ya hapo alihamia timu ya Portsmouth mwaka 2008, ambako alishinda kombe la FA katika msimu wake wa kwanza katika timu hiyo.
Akiwa amenyakua kombe la Ugiriki mwaka 2011 akiichezea timu ya AEK Athens, alirejea England msimu uliopita akijiunga na West Ham.
Aliichezea timu hiyo mara 16 lakini baada ya Desemba hakupatiwa nafasi kubwa ya kuichezea timu hiyo na kuachwa msimu huu wa majira ya joto.
Diop aliiwakilisha Senegal mara nne katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu hiyo iliyofikia hatua ya robo fainali katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2002, zilizoandaliwa kwa pamoja kati ya Japan na Korea Kusini.

   


No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers