Shirikisho la soka nchini TFF limewataka mashabiki wa soka wajitokeze kwa wingi katika uwanja wa Taifa kesho kungalia mchezo mkubwa wa soka kati mabingwa watetezi wa ligi ya soka Tanzania bara Saimba dhidi ya mahasimu wao wakubwa kisoka Yanga, mchezo ambao utapigwa hapo kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akiongea hii leo katibu wa shirikisho hilo Angetile Oseah 'ngeta' amewataka mashabiki kuwa na nidhamu na kuimarisha hali ya usalama na hatimaye kurejea majumbani salama ikiwa ni mchezo ambao unahitimisha super wiki ya supersport.
Mchezo huo umepangwa kufanyika usiku kuanzia saa moja kamili.
Wakati huohuo, TFF kwa kushirikiana na kampuni ya Prime Time Promotion wameamua kuanzisha soka la ufukweni huku TFF ikijipanga kuunda kamati itakayoshughulikia mchezo huo.
Wao Prime time Promotio watakuwa na jukumu la kuutangaza mchezo huo kwa maana ya Promotion mchezo ambao umepangwa kuzinduliwa mwezi wa desemba baada ya mafunzo kutolewa na wakufunzi kutoka shirikisho la soka duniani FIFA mafunzo ambayo yanatarajiwa kutolewa mwezi wa Novemba na kwa kuanzia wataanzia na fukwe za Dar es Salaam na uzinduzi ukitarajiwa kufanyika katika ufukwe wa Coco beach.

ROCKSPORTS
No comments:
Post a Comment