HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

13 November 2012

HARAMBEE STARS YA WASILI TANGU JANA USIKU LAKINI SHILINGI ZA Kenya laki 325,000 (USD 3,200 ZAMFANYA WA NYAMA KUITOSA HARAMBEE STARSS

Kiungo wa kimataifa wa Kenya na Celtic ya Scoitland Victor Wanyama ameshindwa kuja nchini Tanzania na kikosi cha timu yake ya Taifa ya Kenya Harambee Stars kutokana na kile kilichoelezwa kuwa Shirikisho la soka la Kenya Kushindwa kutimiza masharti yake.

Wanyama hapo kabla aliitaka FKF kumrudishia fidia ya nauli yake ya kurudia nchini Scotland ambapo inaarifiwa kuwa ilikuwa ni shilingi za Kenya laki 325,000 (USD 3,200) ambazo zilitokana na mchezo wa oktoba 16 ambapo Wanyama alirejea nchini Kenya kwa ajili ya mchezo wa Harambee Stars dhidi ya Afrika kusini FKF.

Fedha hizo hazikuweza kurejeshwa jambo ambalo halijatekelezwa mpaka leo.
Imeelezwa kuwa familia ya Wanyama imepinga kitendo kama hicho kujirudia wakitaka kwanza kuhakikishiwa juu ya fedha hizo ambapo FKF imetaka kuzirejesha baada ya mchezo na Tanzania.
Amenukuliwa mama yake Wanyama Mildred Ayiemba aking’aka
"hii FA ya Kenya inacheza na mwanagu"

"Victor alipowauliza juu ya pesa yake maafisa wa FA walikuwa wanamzungusha wachezaji wote wanapewa tiketi za kurudia kwanini hivyo kwa mwanangu?"
Harambee Stars iliwasili jijini Mwanza tangu jana usiku majira ya saa nne bila ya wachezaji wake wawili tegemeo Victor Wanyama na Arnold Orig Otieno huku FKF ikishindwa kuieleza TFF sababu za wachezaji kutokufika.
Wachezaji walio wasili ni pamoja na Dennis Oliech, Ayub Timbe Masika, Brian Mandela Onyango (Santos), Patrick Oboya, Mzee Patrick Ooko Osiako, Jerry Santo, Fredrick Jerim Onyango Oduor, Edwin Simiyu Wafula (AFC Leopards) na Eugene Ambuchi Asike (Sofapaka).

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers