HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

25 November 2012

Kutoka kwa Chaurembo Palasa

WANACHAMA,
TANZANIA PROFESSIONAL BOXING COMMISSION,
S. L. POSTA 6058,
DAR ES SALAAM.

Kumb. Na: CP/MO/3 24 Novemba, 2012

Msajili wa Vyama,
Wizara ya Mambo ya Ndani,
S. L. Posta 9223,
DAR ES SALAAM.

Ndugu,

YAH: TAARIFA YA KUFANYA MKUTANO TAREHE 12 JANUARI, 2013.

Rejea barua yako Kumb. Na: S.O. 6446/17 ya 23 Agosti, 2011 iliyotujibu kuhusu mwongozo wa kukufufua chama chetu, kwa kutufahamisha kuwa ombi hilo haliwezi kushughulikiwa kabla haijalipwa ada ya usajili na adhabu ya kutolipa kwa miaka ya fedha 1998 mpaka 2012. Aidha rejea pia barua yako Kumb. Na: S.O. 6446/20 ya
13 Septemba, 2011 iliyosisitiza barua yako Kumb. Na: S.O. 6446/17 ya 23 Agosti, 2011.

Malipo yamekwisha kufanywa na wanachama hivyo tumepanga kufanya mkutano tarehe 12 Januari, 2013 wa kuhakiki wanachama na kufanya uchaguzi wa viongozi wa muda:

[1] UONGOZI WA CHAMA:

Chama hakijawahi kufanya uchaguzi wowote ule kikiwa hai au kimekufa
tangu mwaka 1998 kilipowachagua viongozi :
[a] Emmanuel Salehe – Rais wa chama
[b] Onesmo Ngowi - Makamu wa rais wa chama
[c] Fidel Haynes - Katibu Mkuu
[d] Titus Kadyanji - Mweka Hazina
[e] Habibu Kinyogoli - Mjumbe
[f] Bakari seleman - Mjumbe

Tarehe 12/01/2000 mkutano mkuu wa chama ulimthibitisha Onesmo Ngowi
kama rais wa chama.

Viongozi wote aliochaguliwa 1998 wapo hai kasoro Bakari Selemani ambaye
ni marehemu lakini hawajishughulishi na maswala ya chama. Badala yake
Onesmo Ngowi amekuwa akitoa madaraka anavyotaka yeye hata kwa watu
ambao hawana sifa ya kuwa wanachama. Chama hiki ni cha mabondia.

[2] OFISI YA CHAMA
Chama hakina ofisi wala mahali maalum pa kukutania.

Mabondia wapokuwa na shida huambiwa na Onesmo
Ngowi kuwa wakamtafute Boniface Wambura ambaye kama mwandishi wa
habari hana sifa za kuwa mwanachama.

[3] MIKUTANO YA CHAMA:

Mkutano Mkuu wa mwisho wa chama ulifanyika mwaka 2001 ambao
ulizungumzia mabadiliko ya katiba ambayo ilitaka kuwaondolea mabondia
uwanachama.
Kwa pamoja walipinga hili kwa kuwa hiki ni chama kilichosajiliwa na mabondia
kwa ajilia ya mabondia na wala siyo kampuni ya mtu.

[4] MAPATO NA MATUMIZI:

Taarifa ya mwisho ya mapato na matumizi ililetewa kwa wanachama tarehe
31 Desemba, 2000. ( AMBATANISHO NA: 1 )

Lakini katika miaka yote hii 12 mabondia wamekuwa wakikatwa asilimia kumi
( 10%) ya malipo yao kila waposhindana nje ya nchi aidha mapromota wamekuwa wakilipia vibali vya kuandaa mapambano.

[5] WANACHAMA:

Chama tulikianzisha kwa ajili ya mabondia mwaka 1984 na orodha ya
wanachama mpaka mwaka 1998 ambayo ndiyo iliyofanya uchaguzi wa
mwisho ( AMBATANISHO NA:2 )

[6] DHANA YA KUITISHA MKUTANO
Wanachama tuliona kuwa sababu ya malimbikizo ya ada ya usajili ni kuwa hakukuwa na mtu wa kuwajibika kuhusu hili. Ndio maana tukalipia.

Aidha kukosekana kwa [a] ofisi [b] takwimu ya mapato na matumizi [c]
orodha ya wanachama na [ d] viongozi wa chama wa kuwajibishwa.

Hivyo basi iwapo una pingamizi kuhusu mkutano huu basi tunaomba mwongozo wako.

Wako mtiifu,

_______________ __________________
Chaurembo Palasa Agapeter Mnazareth
MWENYEKITI WA MKUTANO MJUMBE

Nakala kwa: [1] Vyombo vya Habari

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers