HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

24 November 2012

Cecafa: Uganda 1 Kenya 0


Timu za taifa ya Ethiopia na wenyeji Uganda zimefanikiwa kuanza vizuri michezo yao ya Kwanza  ya michuano ya kombe la Challenge iliyoanza hii leo mjini Kampala nchini Uganda.

Hii ni michezo ya kundi  A ambapo mchezo wa mapema timu ya taifa ya Ethiopia ambao mwezi Januari watakuwa wakielekea nchini Afrika Kusini waliiwachapa Sudani Kusini kwa bao 1-0.

Mshambuliaji Yonathan Kebede alifunga bao pekee kunako dakika ya 60 kufuatia mpira wa krosi kutoka mashariki ya uwanja wa Namboole.

Nahodha Leon Khamis alipata nafasi mbili nzuri  kama angezitumia vizuri  wangechomoza na ushindi mnono zaidi.

Hata hivyo kocha msaidizi wa Ethiopia Seyoum Kebede, amesema pamoja na ushindi huo kikosi chake kitalazimika kuongeza jitihada zaidi.

“ni vizuri tumeshinda mchezo wetu wa kwanza wa michuano hii lakini tunalazimika kuongeza jitihada zaidi”.

Katika mchezo wa pili ambao Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Issa Hayatou alikuwa akiushuhudia wenyeji Uganda wamefanikiwa kuanza vema kampeni yao ya kutetea taji hilo wakianza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Harambee Stars ya Kenya.

Mchezaji nyota anayechezea soka nchini Vietnam Geoffrey Kizito alifunga goli hilo pekee zikiwa zimesalia dakika 16 mchezo kumalizika.

Goli hilo lilikuja muda  mfupi baada ya mlinda mlango namba moja wa Uganda ‘The Cranes’ Abel Dhaira akipelekwa katika gari la wagonjwa baada ya kugongana na mlinzi wa Harambee stars katika harakati za kuokoa mpira wa hatari .

Michezo mingine ya kundi A itaendeleea tena jumanne ambapo Ethiopia wataanza mchezo wa mapema dhidi ya Uganda na baadaye Kenya kukutana na Sudani Kusini.

Michuano hiyo itaendelea tena hapo kesho kwa michezo ya kundi B ambapo mchezo wa mapema Burundi wataanza na Somalia na baadaye Kilimanjaro stars watakuwa wakishuka dimbani dhidi ya Sudan.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers