Kocha wa QPR, ambayo kwa sasa iko mkiani kwenye msimamo wa ligi kuu ya Premier ya Uingereza Mark Hughes amefukuzwa kazi.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa bodi ya
wakurugenzi wa klabu hiyo,
kocha huyo amefukuzwa kazi kutokana na matokeo
mabaya tangu kuanza kwa msimu huu.
Baada ya mechi 12 kuchezwa QPR haijashinda hata mechi moja.
Taarifa hiyo imesema kuwa, bodi hiyo inajadili mipango ya kutangaza wasimamizi wapya wa klabu hiyo muda mfupi ujao.
Taarifa hiyo imesema kuwa, bodi hiyo inajadili mipango ya kutangaza wasimamizi wapya wa klabu hiyo muda mfupi ujao.
Mark Bowen na Eddie Niedzwiecki watasimamia
klabu hiyo wakati wa mechi ya ya kesho Jumamosi dhidi ya Manchester
United katika uwanja wa Old Trafford.
''Bodi ya wakurugenzi ingependa kutoa shukrani
kwa Mark, kutokana na juhudi zake wakati akiwa kocha wa klabu hiyo kwa
muda wa miezi kumi iliyopita'' taarifa hiyo iliongeza.
Wakurugenzi hao wamesema watatangaza mipango mipya
ya klabu hiyo muda mfupi ujao na aliyekuwa kocha wa Tottenham Harry
Redknapp anatarajiwa na wengi kuteuliwa kuwa kocha mpya wa QPR.
No comments:
Post a Comment