HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

12 December 2012

Al-Ahly YAKUNG'UTWA 1 NA Corinthians YATUPWA NJE UBINGWA WA DUNIA


Pichani ni Mshabuliaji wa Corinthians  Paolo Guerrero akishangilia mara baada ya kufunga bao la Ushindi katika michuano ya vilabu bingwa ya dunia inayofanyika huko Tokyo japan  Dhidi ya wawakilishi wa afrika Al-Ahly ya Masir alifunga goli hilo kwa kichwa .

Mabingwa wa  America Kusini   Corinthians wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali  ya michuano ya kombe la dunia kwa vilabu  mara baada ya kuifunga Timu ya  Al-Ahly    1-0 mchana wa leo huko   Toyota, Japan.

Kipigo hichi kinaifanya  Al-Ahly's kutupwa nje ya michuano hiyo pasipo wao kutarajia kwani mabingwa hao wa Msiri walikuwa wakicheza bila ya mashabiki kwa kipindi kirefu katika ligi yao ya nyumbani baada ya kutokea vifo vya watu sabini mwezi february huko Port Said .

Goli pekee katika mchezo huo lilifungwa na kijana kutoka Peru   Jose Paolo Guerrero katika dakika ya 29 baada ya kufunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya   Douglas' nje kidogo ya kisanduku cha penati .

Ushindi huu unaama kuwa timu hii kutoka  Sao Paulo itacheza na Na mabingwa ulaya Chelsea kutoka uingereza au Mabingwa wa Amerika ya kati Monterrey ya mexico siku ya jumapili Huko Yokohama .

Corinthians, ni washindi wa kombe la   Copa Libertadores kwa Mara ya kwanza Tangu mwaka 2000 katika historia yao ya hivi karibuni  wakishangiliwa na maelfu ya mashabiki  walisafiri kutoka   Brazil.

Al-Ahly sasa wanatakiwa kuweka nguvu zao siku ya jumapili kwani nafasi yao pekee kwa sasa niku tafuta angalau nafasi tatu katika mashindano hayo   mwaka 2006 mabingwa hawa mara saba wa afrika walishika nafasi ya tatu

Kwa upande mwinge  Corinthians  watakuwa na matumani ya kuwa klabu yao inaweza kurejea yale waliyofanya wakiwa na Mkomgwe wa soka Brazil Romario pale walipotwaa ubingwa huo  katika  ardhi ya  nyumbani

Katika mechi ya mapema  timu mwenyeji ya  Japan's Sanfrecce Hiroshima -- ambao walifungwa na  Al-Ahly katika hatua ya Robo ya  fainali ilikamata nafasi ya tano baada ya kufumua 3-2   Ulsan Hyundai ya  South Korea.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers