HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

4 October 2012

NYANGE,SANGA WALALAMA KUHUS MAAMUZI NA MAPATO



Makamu mwenyekiti wa klabu ya simba amezungumzia kukerwa na mwanuzi wa mechi ya jana kati yao na watani zao wa jadi yanga kwa kuchezesha vibaya mchezo huo ambao ulikuwa ukionyeshwa na kituo cha Runinga cha supersport 9 EAST ambapo baadhi ya matukio yaliyokuwa yakitokea yalistahili kadi nyekundu hasa baada ya Haruna moshi boban kufanya faulo ya makusudi kwa mchezaji wa klabu ya soka ya Dar Es Salaam Young African Mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar Es Salaamm.

SIKIZA HAPA 




Naye Makamu  Mwenyekiti wa klabu yanga Clement akupishana sana na Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya  simba ila yeye alijikita zaidi katika swala mapato ya mechi hiyo ambayo yameingiza shilingi milioni mia tatu tisini huku simba na yanga zikiambulia milioni 90 kila moja na kusema kuwa katika swala mapato bado TFF haijawatendea haki.
 HAPA SIKIZA


CAF YAANZA KUMTAFUTA MFALME WA SOKA AFRIKA MWAKA 2012


Shirkisho la soka Barani afrika (CAF)  limeanza mchakato wa kutafuta mchezaji bora wa afrika kwa mwaka 2012.

huku jumla ya wachezaji 34 watakuwa wakiwania tuzo hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na mchezaji kutoka ivory coast  Yaya Toure.
Ambapo majina 32 ambayo yamepitshwa mpaka sasa wanacheza soka  ndani ya Afrika  Sherehe za kumtafuta Mchezaji Bora wa afrika zinazojulikana kama Glo Caf Gala 2012  zitafanyika Huko Accra Ghana  ,
Mwaka huu wachezaji wa tatu wanaogombania uchezaji bora ni wa zambia wawili  Rainford Kalaba na  Stoppila Sunzu kutoka klabu ya  TP Mazembe huku wakiungana na mchezaji toka Tunisia, Youssef Msakni kutoka klabu ya  Esperance katika uchezaji bora wa afrika ambapo tuzo hii imekuwa ikitawaliwa zaidi na wachezaji ambao hucheza soka nje ya afrika  
ambapo uteuzi wa majina uliegemea zaidi katika uwajibikaji wa wachezaji hao katika vilabu na timu ya taifa 
. CAF itatangaza wachezaji watano bora wanaogombania tuzo hiyo  wanaoacheza soka afrika mwishoni mwa mwezi oktoba kwa kupiga kula na kamati zinazotambulika kiukamalifu na CAF, majina ya wachezaji kumi bora na tano bora yatatumwa kwa vyama husika na kwa makocha wa timu za taifa ilikuchagua wachezaji watatu bora .
Aidha Tuzo zitakazogombaniwa katika sherehe hizo ni 

1.Timu ya Taifa ya Mwaka   

2.Timu bora ya wanawake ya Mwaka   

3.Timu ya Taifa ya Wanawake Ya Mwaka   

4. Klabu bora ya Mwaka 

5.Mchezaji mwenye kipaji kichachovutia   

6. Mkufukunzi Bora wa Mwaka 

7. Mwamuzi Bora wa Mwaka 

8. Tuzo ya Heshima kwa wachezaji wa Zamani 

9. Zawadi ya Ubinadamu kiwanjani 

10. Zawadi  Kwa taasisi au mtu ambaye amechangia maendeleo ya soka afrika au Duniani .

11. Kikosi bora cha Afrika 

Tuzo Kwa  Mchezaji bora wa afrika na kwa Mchezaji Bora afrika anayecheza soka ndani ya afrika .

HABARI YA TANZIA


Bondia bingwa wa taifa wa kilo 59 toka mkoa wa Tanga Said Mundi "smart punch"amefiwa na baba yake mzazi mzee Abdulrahman mbaraka nyumbani kwake Zahrau mkoani Tanga.kifo hicho kilitokea jioni ya jana muda mchache kabla ya Saa moja usiku  ,sababu ya kifo chake cha ghafla inaelezwa ni shinikizo la damu lilitokea kwa muda mfupi na kujaribu kumpeleka katika hospital bombo na kufia njiani, kwa maelezo ya said mundi mwenyewe kwa Ibrahim Kamwe"bigright" ni kuwa baba yake hapo awali hakuwa na ugonjwa huo umekuja ghafla na umemchukua baba. Wanategemea kuzika leo jioni.

Said Mundi anaetegemea kupanda ulingoni tarehe 26 octoba 2012 kuzichapa na jumanne Mohamed raundi kumi kugombania ubingwa wa PST katika uwanja wa mkwakwani-Tanga.viongozi wote wa masumbwi kwa pamoja wapo  pamoja na said mundi katika wakati huu mgumu uliompata na tunashirikiana katika shughuli nzima za kufanikisha msiba huu.Mungu ailaze roho ya mzee Abdi Mbaraka mundi peponi - amin

CAF YABADILI RATIBA KLABU BINGWA AFRIKA

Shirikisho  la soka la Afrika CAF Limetangaza mabadiliko ya Tarehe za mechi ya  fainali ya mkondo wa pili,  CAF imesema imeamua kubadili ratiba ya mechi namba  116 (2ND ya fainali mkondo wa pili  ya klabu bingwa Barani afrika  2012, ichezwe mwishoni mwa juma la Tarehe  16th, 17th au 18th mwezi 11 2012  Tofauti nailivyokuwa mwanzo (9th, 10th au 11th Mwezi wa 11   2012).

Mabadiliko haya yamekuwa ya kipekee kutokana kuingaliana kwa ratiba na michuano ya soka kwa Wanawake kwa afrika ambayo itafanyika  (kuanzia Tar  11th  Nov.2012) na itawapatia muda wa kupumzika wa majuma  mawili timu zilizoingia fainali katika mechi zote mbili   za fainali. 

YANGA NA SIMBA ZAINGIZA MPUNGA WA MIL 390/=


Pambano la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.

Watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.

Umeme sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.

Wakati huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000 imeingiza sh. 27,000.

Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na DRFA sh. 915.2

RAMSEY KAFUNGA JE ZAMU YA NANI KUONDOKA

Mshambuliaji wa arsenal Gervinho akishangilia goli la kwanza la timu ya dhidi ya olympiacos ya ugiriki.

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers