Azam FC inaendelea na maandalizi ya siku saba jijini
Nairobi, kesho watacheza mchezo wake wa pili dhidi ta SOFAPAKA ya Kenya kwenye
Uwanja wa Nyayo.
Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema mechi
itakuwa nzuri kwake kutokana timu hizo kucheza mchezo wa aina inayofanana baada
ya kuzifundisha timu hizo.
Stewart alisema mechi hiyo muhimu kwake itakuwa na
sura tofauti kwa kukutanisha wachezaji walipata mafunzo kupitia kwake, hivyo
mbinu na aina nyingine ya mchezo bado SOFAPAKA wanaitumia.
"Nataraji kuona wachezaji wangu wote wakifanya
vizuri hasa wa Azam FC, kupambana na timu uliyoifundisha kunakuwa na ugumu,
wanaweza kucheza wakifanana kila sehemu hali itakayopunguza idadi ya magoli kwa
moja timu hizo” alisema Stewart.
Alisema wachezaji wake wanaonekana kucheza vizuri
kipindi hiki, wamezoea hali ya hewa Nairobi hivyo mchezo na SOFAPAKA watakuwa
na kila sababu ya kufanya vizuri.
Naye Kocha wa SOFAPAKA David Ouma alisema kukutana
na Azam FC katika mechi ya kirafiki ilikuwa moja ya mipango yao, wanatajia
kucheza mchezo wa ushindani zaidi na kuwapa nafasi wachezaji wake wapya
walisajiliwa hivi karibuni.
“Haya ni maandalizi mazuri kwa timu yangu, tumeanza
mazoezi wiki mbili zimepata, kupitia mechi hii tutajua maendeleo ya timu,
wachezaji hasa hawa tuliowasajili, pia tutazidi kujenga urafiki mzuri na Azam
FC” alisema kocha Ouma.
Azam FC baada ya mchezo huo, siku ya Jumatatu
itapumzika kwa kufanya mazoezi, na kumaliza mchezo wake wa tatu siku ya Jumanne
dhidi ya K.C.B utakaochezwa kwenye Uwanja wa City uliopo jijini hapa.
Timu hiyo inatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam
siku ya Jumatano ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa ligi kuu Tanzania
mzunguko wa mwisho wa ligi utakaoanza Jan 26 mwaka huu.
Mwisho
Contacts
Ass. Manager Jemedari Said
+255 713528790
No comments:
Post a Comment