AZAM FC Imefanikiwa kutetea Kombe la Mapinduzi usiku WA Kuamkia Leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao
2-1.
Kwa ushindi huo, Azam wamezawadiwa Sh. Milioni 10, wakati
washindi wa pili Tusker wamepata Sh. Milioni 5.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Ramadhan Rajab Ibada
‘Kibo’ aliyesaidiwa na Mwanahija Makame Mfumo na Mgaza Kindundi, hadi mapumziko
hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.
Gaudence Mwaikimba alipewa pasi
nzuri na Brian Umony dakika ya 44, lakini shuti lake kali lilidakwa na kipa
Samuel Odhiambo.
Kipindi cha pili, Tusker walirudi na moto mkali na kuanza
kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Azam,
na iliwasaidia mabingwa hao wa Kenya kupata bao dakika ya
60, lililofungwa na Jesse Were aliyeunganisha kwa shuti kali pasi ya Robert Omunok
, bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC
walisawazisha dakika ya 72 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na beki Mkenya,
Joackins Atudo baada ya beki wa Tusker, Luke Ochieng kuunawa mpira kwenye eneo
la hatari.
Katika dakika mbili za nyongeza baada ya kutimia dakika
90 za mchezo huo, alijitokeza binti mwenye umri kati ya 14 na 16 na kukatiza
uwanjani akitokea jukwaa la Urusi.
Refa alijaribu kumsimamisha, lakini aliendelea kukatiza
Uwanja hadi nje ambako alipokewa na askari Polisi na kutolewa nje kabisa ya
Uwanja. Mtangazaji wa Uwanja wa Amaan, Farouk Karim aliwatuliza mashabiki
akisema binti huyo ametoroka hospitali ya ugonjwa wa akiri , iliyopo Kidongo Chekundu na tayari
Polisi wamemkamata na kumrejesha huko.
Hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana
bao 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30.
Gaudence Exavery Mwaikimba aliipatia Azam bao la ushindi
dakika ya pili tu tangu kuanza kwa muda wa nyongeza baada ya kuwazidi nguvu na
maarifa mabeki wa Tusker.
Bin zuberyblog
Bin zuberyblog
Safi Azam
ReplyDelete