Tamasha
la Muziki la Sauti za Busara kwa mwaka huu litafanyika eneo la mji mkongwe
Zanzibar, kuanzia tarehe 14 hadi 17 Februari, jitihada zimefanyika katika
kufanikisha tamasha la 10 na kuhakikisha kuwepo kwa uhuru wa kujieleza kupitia
nyimbo mbalimbali za wasanii
wa Kiafrika ambao nyimbo zao zimepigwa marufuku au kuzuiwa katika nchi
wanazotoka.
Kutakuwa
na waimbaji wengi mahiri, akiwemo muimbaji mwenye misimamo kutoka jamii
ya kiisilam nchini Mali, anaejulikana kwa jina la Khaira Arby ambae alifungiwa
kuimba licha ya kwamba nyimbo zake zinamsifu/ elezea Mtume Mohammad (SAW).
Mwengine ni Comrade Fasto anayetoka Zimbabwe,
msanii mahiri wa kurap na mshauri, ambae nyimbo zake zinakosea serikali ya
Mugabe hali iliyopelekea nyimbo zake kutopigwa katika radio na Televishen ya
taifa. “Tuna uwezo wa kufikisha ujumbe wetu kwa walengwa. Tuna timu
nzuri( mitaani) zenye uwezo wa kusambaza kopi nyingi za albam katika maeneo
mbalimbali na hata katika mabasi ya abiria ambayo mengi
yanatumiwa na wazimbabwe wa kawaida. Tumebuni njia mbadala “Radio Watu” na
albam imekuwa zikichezwa katika vyombo mbalimbali vya usafiri”. Alisema
Comrade Fasto.
Wakati
wa kongamano lijulikanalo kama Movers & Shakers ya Sauti za
Busara, jopo la wasanii litafanya majadiliano ya kuangalia umuhimu wa kulinda
uhuru wa kujieleza kwa wasanii. Nae Rebecca Corey, Mkurugenzi Mtendaji
wa Busara Promotions anaamini kwamba ni muhimu kwa wasanii kupata nafasi ya
kupaza sauti zao. “Muziki ni njia moja yenye nguvu, lazima tuseme hali ya
kutokuwa na usawa, tufurahie maisha, na kueleza hali ya utu wa mtu. Uhuru wa
kujieleza ni haki za binadamu, na unatunufaisha sote ikiangaliwa na
kuheshimiwa. Ndio maana Sauti za Busara ina jivunia kukuza sauti za wasanii
kama Khaira Arby na Comrade Fasto ambao wamepigwa marufuku katika nchi wanazotoka”.
Msanii
Khaira Arby kutoka Mali atafanya onesho lake katika tamasha la 10 la Sauti za
Busara siku ya mwisho ya tamasha litakaloanza tarehe 14
hadi 17 Februari pale Ngome Kongwe, Zanzibar. Akivutiwa
na binamu yake Ali Farka Toure, Khaira Arby katika muziki wake ameweka
vionjo vya chimbuko la Berber na Songhai ambapo umekuwa ukileta
mchanganyiko mzuri wa kuvutia wa desert blues na wakati wa kurikodi
huchanganya na kinanda cha guitar la umeme, ngoni, ngoma na muziki wa
kitamaduni na kuufanya mziki wake uvutie sana. Arby, amezaliwa katika kijiji ambacho
hakipo mbali na mji wa Timbutku, ambao umezungukwa na jangwa.
Kwa upande mwingine, Samm Farai Monro, anaejulikana zaidi kama Comrade
Fatso, ni mmoja wa msanii ambae ni maarufu na
anavuma kwa mashairi Zimbabwe. Anaimba mashairi ya Toyi Toyi, mashairi ya
mtaani yenye msimamo ambayo anachanganya na lugha ya Shona na kiingereza na mbira pamoja na hip hop. Atafanya
onyesho lake sambamba na kundi la Tanzania Mlimani Park Orchestra wajulikanao
pia kama Sikinde, Atongo
Zimba kutoka Ghana, N'Faly
Kouyaté kutoka Guinea, Owiny
Sigoma Band kutoka Kenya, pamoja na wazimbabwe wenzake Mokoomba.
Miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania watakao shiriki katika
tamasha la mwaka huu ni pamoja na Msafiri
Zawose na Sauti Band, Lumumba
Theatre Group, Super Maya
Baikoko, Peter
Msechu na wengineo wengi..
Kiingilio kwa watanzania ni shilingi 3,000 na kiingilio
maalumu kwa wakaazi wa Africa Mashariki.
Kwa
maelezo zaidi na picha downloads: Tafadhali
tembelea wovuti ya www.busaramusic.org
No comments:
Post a Comment