Bondia
Iddy Mnyeke kulia akioneshana umbwamba wa kutupiana masumbwi na Mussa
Sunga wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala Dar es
salaam jana Mnyeke anajiandaa na Mpambano wake zidi ya Sadiki Momba
February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam
BONDIA Iddy Mnyeke yupo katika maandalizi mazito ya kujiandaa na mpambano wake na Sadiki Momba utakaofanyika February 14 katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam
Bondia huyo kwa sasa ananolewa na kocha wa kimataifa wa Mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo wameweka kambi ili kumkabili Momba
Akizungumza Super D alisema kuwa amemwingiza kambini bondia wake ili aweze kumtengeneza vizuri kwa ajili ya mpambano wake na Sadiki Momba
Super D alisema kuwa mpambano huo utakuwa wa utangulizi kabla ya Deo Njiku na Omary Ramadhani kutwangana kugombea Ubingwa wa Taifa wa PST
Kocha huyo alisema kuwa kambi yao itahakikisha inaendeleza ubabe baada ya bondia tegemeo wa kambi hiyo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kumdunda Saidi Mundi Kutoka Tanga
Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina. michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana

No comments:
Post a Comment