HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

17 January 2013

NAKARIBIA ULAYA SASA!!!


 http://kandanda.galacha.com/wp-content/uploads/2013/01/emmanuel-okwi_3601.jpg

 Mshambuliaji mpya wa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia, Emmanuel Okwi, amesema kwamba kusajiliwa kwake na klabu hiyo ambayo ni moja ya klabu vigogo barani Afrika ni dalili njema  na anaamini kuwa sasa amebakiza hatua chache kuufikia mlango wa kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Simba imemuuza kwa Etoile mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda kwa dau la dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 470). Etoile ni mabingwa wa Afrika mwaka 2007.

  Amesema  kwamba sasa anaiona Ulaya iko karibu zaidi kwake na kwamba, anachotakiwa kufanya ni kuendelea kucheza soka kwa kiwango cha juu na kuzingatia nidhamu ya mchezo huo.

Okwi amesema kuwa baada ya kukosa timu Austria mwaka jana,  kamwe hakuweza kukata tamaa na anamshukuru Mungu kwamba ubingwa wa mashindano ya Kombe la Chalenji yaliyomalizika mwaka jana jijini Kampala ulimsaidia kuimarisha kiwango chake na kwenda kwenye majaribio akiwa fiti.


"Ewe Mungu, nakushukuru kwa kuniwezesha kutimiza malengo yangu katika kiwango cha juu, bila ya wewe nisingeweza kufika hapa nilipo sasa," aliongeza Okwi, akirejea kile alichoandika juzi kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa facebook.


Nyota huyo aliyezaliwa Desemba 25 mwaka 1992, aliongeza kwamba kila anachokifanya na hatua anazizifikia katika kucheza kinatokana na juhudi zake na maombi anayoyafanya kila anapomaliza mazoezi.



Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, ndiye aliyekwenda Tunisia kukamilisha mazungumzo ya kumuuza mchezaji huyo na kusema kwamba tayari taratibu za uhamisho zimekamilika.

Rage amesema  kuwa katika mkataba ambao Okwi amesaini, Simba itaendelea kufaidika ikiwa Mganda huyo atauzwa kwa klabu nyingine.

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers