Kumbukumbu Na.
TFF/ PRESS/ADMN.13/7 Januari 14, 2013
WAHARIRI
VYOMBO VYA
HABARI
DAR ES SALAAM
YAH: SEMINA YA
KANUNI ZA UCHAGUZI TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina
kuhusu Kanuni za Uchaguzi za TFF itakayofanyika Jumatano, Januari 16 mwaka huu
kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana kwenye ofisi za TFF.
Semina hiyo itashirikisha Wahariri (Editors), Wasanifu Kurasa (Sub
Editors) na Waandishi (Reporters). Unaombwa kuzingatia muda ili kufanikisha
semina hiyo.
Wako katika michezo
Angetile Osiah
KATIBU MKUU
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU
TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment