Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) utafanyika Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari imefanya uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano uliowaingiza madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya keshokutwa (Januari 17 mwaka huu).
Mkoa utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao ni Oscar Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao wanaowania ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

No comments:
Post a Comment