Timu ya Young Africans imeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa
Kijitonyama mabatini kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya
vodacom na mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopard kutoka
nchini Afrika Kusini siku ya jumamosi mchezo utakaofanyika katika Uwanja
wa Taifa jijiji Dar es salaam.
Young Africans ambayo imerejea siku ya jumatatu alfajiri ikitokea
nchini Uturuki ambako ilikuwa imeweka kambi ya mafunzo kwa takribani
wiki mbili, iliwapa wachezaji wake mapumziko ya siku mbili kabla ya leo
tena wachezaji wote kuanza mazoezi.
Wachezaji wote waliokuwa na
timu katika kambi ya mafunzo nchini Uturuki wameanza mazoezi huku umati
wa watu wengi ukijitokeza kuwaona vijana wa Jangwani ambao tangu warejee
nchini leo ndio ilikua wanaanza mazoezi katika ardhi ya nyumbani.
Mchezo
wa jumamosi dhidi ya timu ya Black Leopard utakua ni mchezo wa kwanza
kwa Young Africans katika aridhi ya nyumbani katika mwaka mpya wa 2013
hivyo watatumia fursa hiyo kuwaonyesha washabiki ufundi walioupata
kutokana na kambi hiyo ya mafunzo mjini Uturuki.
Timu ya Black
Leopard inatajiwa kuwasili siku ya alhamis asubuhi ikitokea nchini
Afrika Kusini tayari kabisa kupambana na mabingwa mara 23 wa ligi kuu ya
Tanzania bara na mabingwa mara tano (5) wa kombe la Kagame.
Yanga
itaendelea na mazoezi yake kesho asubuhi katika uwanja wa Mabatin
Kijitonyama kujiandaa na mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mzuri wenye
upinzani na wakuvutia ikizingatiwa timu ya Yanga ilikuwa kambi ya
mafunzo nchini Uturuki ambao ilipata nafasi ya kuwa pamoja na mwalimu
kuwafundisha wachezaji wake pamoja.
Viiingilio vya mchezo huo ni
Tsh 30,000/= VIP A, Ths 20,000/= VIP B, Tsh 15,000/= VIP C , Tsh 7,000/=
Orange na Tsh 5,000/= Blue & Green.
No comments:
Post a Comment