Klabu ya soaka ya Arsenal' ipo katika hari mbaya zaidi hasa katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya huku matumani yao ya kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2005 yakionekana kupotea kama si kuzimika baada ya kukung'utwa katika uwanja wa Emirates ambao ni nyumbani kwa klabu hiyo ya arsenal .
Arsene Wenger aliwataka wachezaji wake kuonyesha uwezo mara baada ya kufungwa na kusukumwa nje ya kombe la FA katika uwanja huo huo wa nyumbani dhidi ya timu ya daraja la chini ya blackburn Rovers ambapo pia ilikwisha tolewa katika kombe la capital dhidi ya timu ya daraja la pili ya Bradford
Viongozi wa Bundesliga Bayern hawakuwa na muda wa kupoteza mara tu mpira ulipo anza na kujifaidisha mapema na magoli ya ugenini huku mechi ya marejeano ikifanyika katika kiwanja chao cha nyumbani cha katika hatua ya kumi na sita bora cha Allianz Arena.
Toni Kroos na Thomas Mueller waliipatia Bayern faraja baada ya kuapachika magoli ya haraka haraka japokuwa Lukas Podolski alirejesha goli moja katika kipindi cha pili , Mario Mandzukic's alizamisha bao la tatu na hivo kuifanya arsenal kusubiri miujiza huko ujerumani.
Arsenal walionyesha kila aina ya juhudi lakini Bayern walitumia akiri na uzoefu na uwezo wa hari ya juu, lakini kwa sasa inaoneka kuwa arsene wenger atakuwa anapigania nafasi ya nne na ndio litakuwa lengo muhimu kwake .
safu ya ulinzi ya arsena ilijitahidi kufanya wawezalo huku ikitegemea uwezo wa mshambuliaji kinda wa ambaye anageweza kuisumbua klabu ya Bayern ambayo ilibdi ikwaane mshambuliaji Theo Walcott. lakini hakuweza kufua dafu mbele yao kwani ndani ya 21 arsenal ilikwisha umia
.
Kroos aliachia mkwaju mkali katika dakika ya saba pale alipoachwa peke yake nje ya kisanduku cha arsenal na akafunga goli malidadi kwa lugha ya kitaalamu ( volley) shuti hilo kali lilimshinda mlinda mlango wa arsenal
Wojciech Szczesny.
Mashabiki wa arsenal walijarijabu kuipa moyo timu yao lakini siku haikuwa ya kwao kwani Bayern walizidi kulisakama goli la arsenal . Szczesny alijaribu kutaka kumdanya Daniel van Buyten's alipiga mpira kwa kichwa ambao ulikwenda juu ya mwamba wa goli lakini Mueller alimzidi ujanja Mikel Arteta na kufunga goli
Vijana wa Wenger' walichanganyikiwa na walianza kucheza vibaya huku
Bacary Sagna, Thomas Vermaelen na Arteta, wakiambulia kadi ya njano
Gunners ilijitahidi kuonyesha uwezo lakini nguvu ,na uimara wa Bayern uliwazidi kete arsenal .Ndipo mario
Mandzukic alipomaliza ubishi na kufunga bao la tatu hatua chache akiunganisha krosi ya Nahodha Philipp Lahm's kutoka upande wa kulia .
Arsenal ilibidi kukaza buti inavyotakiwa dakika kumi baada ya kipndi cha pili kuanza Podolski alifunga goli kwa kichwa baada ya mlinda mlango wa Bayern , Manuel Neuer kushindwa kucheza mpira wa kona .
Goli hilo
liliwapa arsenal matumaini ya kurejea mchezo na kocha wa timu hiyo alifanya mabadiliko huku zikiwa zimesalia dakika 19 mpira kumalizika Olivier Giroud an Tomas Rosicky waliingia badala ya Podolski na Aaron
Ramsey.
Giroud alimanusura asawazishe akicheza mpira wake wa kwanza shuti hilo liliokolewa na mlinda mlango hatari Neuer.
mashabiki wa arsenal walidhani kuwa wangesawazisha goli lakini bayern iliongeza bao la tatu
.Bavarian walifanya mabadiliko kwa kuingiza Arjen Robben, ikimtoa Franck Ribery, akicheza nyuma ya nahodha Lahm ambaye naye akufanya ajizi kumtafuta Mandzukic,alieukandamiza bao la tatu kumaliza kabisa ndoto za arsenal kufika japo robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya .
FC Porto
1 Joao Moutinho
Malaga
0
No comments:
Post a Comment